Msanii Nikki wa Pili amedai kuwa watanzania wengi hawajapata elimu
kutokana na kuwa mfumo wa elimu Tanzania unabagua watu na ndiyo maana
hata wasanii wengi hawajaenda shule na siyo kwamba hawapendi shule.
Nikki
amefunguka hayo na kusema kuwa mchakato wa michujo inayotumika kupata
wasomi imekuwa ikiwatenga wanafunzi wenyewe na hali hiyo inasababishwa
na...
elimu inayotolewa ili kumkuza mwanafunzi.
Nikki amesema kwamba licha ya
kulalamikiwa wanafunzi wanalega shule ni kutokana na kukosa mfumo bora
wa kuwapelekea wao kutimiza ndoto zao zaidi ya kukaririshwa kuhusu
elimu.
"Nikienda shuleni sasa hivi
nikimuambia mwalimu anipe wanafunzi 10 wenye akili ataniletea anayejua
hesabu, physics na masomo mengine lakini sitaletewa mwanafunzi anayejua
kuchonga au anayejua muziki 'so' ikifika hapo unakuta mwanafunzi
mwenyewe anaamua kufuata kile ambacho anaona anakiweza. Hivyo kwa mfumo
huu hata wasanii wengi unakuta hawaendi shule" , amesema Nikki.
Aidha Nikki ameongeza, "Mtu
kama Joh Makini na Rama Dee wana elimu za muziki ambayo wamejifunza,
hivyo lazima watafanya vizuri, tofauti kama wangekuwa wanafanya kitu
ambacho hawakipendi.
0 comments:
Post a Comment