Pages

Subscribe:

Tuesday, September 12, 2017

PRODUCER JACK JACK AJIUNGA NA LEBO YA KAKA EMPIRE



Lebo maarufu ya muziki nchini Kenya, Kaka Empire inayomilikiwa na King Kaka imemsaini mtayarishaji wa muziki maarufu nchini humo, Jack Jack On The Beat. Mmoja wa viongozi wa lebo hiyo, ameiambia Bongo5, Jack atakuwa ndio mtayarishaji mkuu katika studio ya Kaka Empire Studios.

Naye mtayarishaji huyo baada ya kusaini mkataba huo amesema, “Kujiunga na Kaka Empire ni uamuzi bora zaidi ambao...
nimeufanya mwaka huu. Wakati fulani katika maisha mtu unatakiwa kujiunga na timu ya kushinda.”

Jack ameshawahi kutayarisha ngoma kibao kali ikiwemo Tippy Toe, Bazokizo, Zigwembe, Sema Ng’we na nyingine.

0 comments:

Post a Comment