BARNABA: DIAMOND SI MWANAMUZIKI WA KWELI ANAIMBA KIUJANJA TU
Jana, Wakati akihojiwa na Mwanadada Shadee kwenye Kipindi cha Clouds E
cha Clouds TV, Msanii 'Fundi wa Muziki' kutoka nyumba ya vipaji THT,
Barnaba Elias 'Barnaba', pamoja na mambo mengi aliyozungumzia, alitoa
maelezo kuhusu wasanii watano anaowakubali na sifa zao Kimuziki ambapo
alimtaja Msanii wa BongoFleva Diamond Platnumz kuwa sio 'Mwanamuziki'
mwenye kujua kuimba muziki kiufundi.
Akifafanua kauli yake kwa mapana , Barnaba alieleza kwamba... Diamond hajui
kuimba kufuatana na alama zote muhimu za muziki, bali hutumia mtindo
flani wa kuimba 'kiujanja', mtindo ambao kwa wanaojua kuimba muziki
technically huwa wanautumia pale wanapofeli kufuata kanuni za uimbaji
wakati wakiimba. Hata hivyo, alimsifia kwa kuwa 'mjanja' na kuweza kufanya muziki wake kuvutia na kuleta ladha. Orodha ya wasanii ambao aliwatolea maoni na kusema ni wasanii
anaowakubali sana ni pamoja na, Diamond, Ally Kiba, Ditto, Amini na yeye
mwenyewe.
No comments:
Post a Comment