Kijana mmoja nchini Ghana huenda akakatwa kidole chake baada ya pete
aliyoiokota na kuivaa kung’ang’ania kwenye kidole ambacho kimeshaanza
kupuputika huku nyama zikianza kuliwa kimaajabu na kuanza kumtia hofu
kijana huyo. Kijana huyo aliyefahamika kama Eric Buageng, alisema niliiokota pete hiyo
pembeni ya barabara wakati... akirudi nyumbani akitokea Kanisani na kuivaa
kwenye kidole cha shahada mkono wa kulia, lakini cha kushangaza baada
ya kufika nyumbani alianza kusikia maumivu kutokana na pete hiyo kumbana
kidole.
Eric amesema kilichomshangaza zaidi ni wakati alipokuwa anaiokota mkono
wake ulikuwa ukitetemeka na alipojaribu kuitupa hakuweza na kusikia
sauti ambayo hakujua ilipotokea ikimwambia aende nyumbani, alipofika
alijaribu kuitoa lakini hakuweza na kuna wakati anakisikia sauti
ikumuamuru atoke nje lakini haoni mtu yeyote.
Tangu wakati huo jitihada za kujaribu kuitoa pete hiyo zimeshindikana
pamoja na kwenda kwenye Hospitali mbalimbali ikiwemo ya wataalam wa
Jeshi ya 37’ Military na ile ya Korle Bu Teaching bila mafanikio, katika
jitihada za kuhakikisha inatoka alikutana na wachungaji mbalimbali
waliomuombea lakini hakufanikiwa kuitoa.
No comments:
Post a Comment