Staa mdogo kwenye kiwanda cha filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’
ameonekana kumrushia vijembe hasimu wake mkubwa mlimbwende Husna Maulid
kwa kile alichodai kuwa anamuibia maelezo yake ya picha (caption) kwenye
mtandao wake wa Instagram. Staa huyo ambaye hakumtaja Husna moja kwa moja, alisema kwa sababu
amekuwa akiweka maelezo ya picha katika mtandao na mtu kuyaiba kama
yalivyo na kuweka katika picha zake, ameamua... kutoa onyo ili asiibiwe.
“Naweka caption lakini ina hati miliki, wewe unayechukua na kuhamishia
kwako, tafadhali.” Aliandika Lulu mtandaoni ambapo alipoulizwa na
mwandishi wetu kama alimtupia vijembe Husna, alisema:
“Jamani sijataja jina la mtu yoyote lakini kama kuna ambaye anajihisi basi ndio huyohuyo.”
Husna amekuwa akikopi maneno ambayo Lulu anayaweka katika kurasa zake
kama: “You can copy my things but you can’t be me.” Husna naye anaandika
hivyohivyo.
Wawili hao waliwahi kuwa marafiki kisha kutofautiana wakituhumiana kuibiana bwana.
No comments:
Post a Comment