Yamekuwa hayo? Aliyewahi kuwa mwandani wa staa wa Bongo Fleva Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’, Penniel Mwingilwa `DVJ Penny’ amegoma kuulizwa
chochote kuhusu kitendo cha zilipendwa wake huyo kupata mtoto wakati
yeye alidaiwa kukataa kumzalia.
Akizungumza wikiendi iliyopita, Penny alifunguka
kwamba, haoni kama kuna sababu ya kumzungumzia Diamond na mtoto wake
(Tiffah) kwani... walishaachana zaidi ya miaka miwili sasa.
“Jamani, huyo mtu kwa sasa hanihusu na sioni kama kuna sababu ya
kumuongelea mtoto wake, anayepaswa kuulizwa mambo ya Diamond ni Zari,
kwa hilo mnisamehe (no comments), nikiulizwa niulizwe mambo yangu tu,” alisema Penny.
No comments:
Post a Comment