ZARI AWAJIBU IVAN NA KING LAWRENC ''VISASI HUFANYWA NA VILAZA''
Hatimaye Zari The Bosslady ameamua kumjibu ex wake Ivan na swahiba wake
King Lawrenc ambao wamekuwa wakimtupia madongo kuwa mtoto wake Tiffah si
wa Diamond, ni wao. King Lawrence alienda mbali zaidi kwa kutumia kampuni ya wanasheria
kumtaka achukue vipimo vya DNA vya kichanga hicho chenye zaidi ya
followers 80k kwenye Instagram.
Zari ametumia Instagram kuwajibu kwa kudai kuwa wanachofanya wawili hao ni visasi ambavyo anaamini... hufanywa na vilaza!
“Visasi hufanywa na vilaza,” ameandika Zari kwenye Instagram.
“BO$$LADY anafahamu kuwa huzuni aliyonayo mtu mwenye chuki wakati
akiangalia furaha na mafanikio yake ni adhabu tosha. Inabidi niyageuzie
mgongo mambo yate ya kijinga yanayoendelea. Naendelea kuwaua kwasababu
watu hutaka kuzima taa inayowaka zaidi kwao,” ameongeza.
Diamond tayari ametoa majibu yake kufuatia hatua hiyo ya Ivan na Lawrenc.
No comments:
Post a Comment