MUUZA nyago kwenye video za Kibongo, Gift Stanford ‘Giggy Money’
amefunguka kuwa mtangazaji maarufu Bongo anayeuza maneno katika Kituo
cha Redio cha Clouds FM, Gardner G. Habash hachomoki kwake na hadi sasa
wako kwenye uhusiano wa mapenzi kwa muda wa miezi sita, Akichonga na mwandishi baada ya picha zinazomuonesha akiwa kwenye
mapozi ya kimahaba na Gardner kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, Giggy
alisema... mtangazaji huyo amekuwa mtu wa muhimu kwake kwa sasa.
“Kwani kuna tatizo nikiwa na Gardner? Yule ni mtu muelewa na sahihi
kwangu, ninafikiri kupitia yeye nitajifunza mambo mengi na kuzidi
kufanikiwa kwa sababu yeye ni moja kati ya watu ambao wako kwenye tasnia
ya burudani kwa muda mrefu,” alisema Giggy Money.
Gazeti hili lilimtafuta pia Gardner ili aweze kufungukia ubuyu huo, alipopatikana alisema;
“Nipo karibu na Giggy lakini hatuna uhusiano wa kimapenzi, kwa hiyo kama
anasema hivyo si kweli lakini yeye ni shabiki wangu na mimi ni mshabiki
wake, ninapenda pia kazi anazozifanya,” alisema Gardner.
No comments:
Post a Comment