skip to main |
skip to sidebar
ESMA PLATNUMZ: NAMSHANGAA DIAMOND KUWA NA CHUKI KIASI HIKI KWA BABA MZAZI
Dada wa ‘kichaa’ wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma
amemshangaa kaka yake, (Diamond) kwa kuendeleza chuki dhidi ya baba yake
mzazi, mzee Abdul Jumaa. Akizungumza na mwandishi kwa njia ya simu
hivi karibuni, Esma alisema siku zote si vyema kukaa na... kinyongo au
chuki dhidi ya wazazi na hata kama ikitokea ni vyema kuyamaliza kwa
mtoto kujishusha.
“Hata mimi nilishawahi kukosana na baba yangu, lakini nilishasamehe
na kusahau kabisa, hata hapa nyumbani, ni mara nyingi tu huwa
tunatofautiana na mama lakini hata kama yeye kakosea, huwa najishusha si
kama ilivyo kwa Nasibu (Diamond) kuwa na chuki kali kiasi hicho dhidi
ya baba yake,” alisema Esma.
0 comments:
Post a Comment