Monday, March 27, 2017
LOVE STORY: SLAVE SEX (MTUMWA WA NGONO) 01
SLAVE SEX(mtumwa wa ngono)
Sehemu ya kwanza
AGE…..(18+)
******
Jasho lilizidi kumtoka Mzee Alex Mwandambo!hasira zilimpanda maradufu, mapigo yake ya moyo yalimwenda mbio,kifo cha kuteseka ndicho kitu alichokuwa anakifikiria kichwani mwake huku akiwa katika kasi ya ajabu akiendesha gari lake usiku wa saa saba kurejea nyumbani kwake, alishaelewa nini maana ya ugonjwa hatari wa virusi vya UKIMWI unavyotesa kabla ya kukutowesha duniani,aliona bora afe haraka kuliko kufa na kifo kibaya kama hicho, alijilaumu sana kuisaliti ndoa yake.
alimlaumu shetani siku zote. Watoto wake Jamal na Mackline aliwaonea huruma sababu bado walikuwa wadogo mno kukosa mapenzi ya baba yao. Alifika nyumbani kwake Afrikasana na...
kuweka gari getini kabla ya kuingiza gari ndani.Geti likafunguliwa na mlinzi.
“Noo! Hapana lazima nikumalize Hafuani,siwezi kukuacha uendelee kuishi duniani”Alisema.
Hapo ndipo Mzee Alex Mwandambo alipogeuza shingo yake nyuma na kuanza kurudisha gari kinyume nyume na kulitoa kwa kasi kama mtu aliyechanganyikiwa,alitetemeka kwa hasira,Msichana mdogo aliyemuambukiza ukimwi hakutaka kumuacha hai,alitaka kumuua,hiyo ndiyo aliamini kuwa ingekuwa adhabu ya binti huyo ambaye atakaye ukatisha uhai wake.
Kifupi Mzee Alex Mwandambo alikuwa mfu aliye hai na hivyo ndivyo alivyoamini tangu apewe majibu hayo wiki nne zilizopita.
Alivyofika Mwenge mataa alikunja kulia na kuchukua barabara inayokwenda Ubungo baada ya dakika kumi baadaye alifika maeneo ya chuo kikuu cha UDSM bado alikuwa katika mwendokasi uleule,alivyofika kituo cha polisi alikunja kona na mbele kidogo kulikua kuna msitu wenye giza na miti mingi,aliweka mguu kati na kupiga breki za ghafla na kufanya vumbi litokee na kuonekana japokuwa kulikuwa kuna giza totoro,kutokana na hasira alizokuwa nazo alishuka garini bila ya kufunga mlango huku gari likiwa bado linawaka, linamulika! taa za mbele hazijazimwa.
“Wewe Malaya bado haujafa tu?”
Hilo ndilo swali la kwanza kulitupa kwa msichana aliyekuwa amefungwa kwenye mti na kamba za katani amezungushiwa mwilini.
Licha ya kufungwa kwenye mti huo kwa siku mbili bila kupata matunzo lakini bado alikuwa mzuri,alikuwa mweupe wa kung’aa mwenye midomo milaini pamoja na macho makubwa ya kusinzia.Kwa harakaharaka ungemtizama ungedhani wenda ni ‘Africast’
“Al…ex niu..e basi”
“Utafia hapo hapo mtini,kwanini lakini hukuniambia kama wewe ni muathirika,kwanini?hukujua kuwa nina familia?nakuuliza wewe Malaya mbwa?”
“Nilishawahi kukwambia nakumbuka,lakini kwa tamaa zako ukaamua kunibaka”
“Kukubaka?kwanini hukukataa sasa?hata ivyo lazima nikuue leo,baada ya hapo namimi natoweka duniani,siwezi kufa kifo cha mateso”
“Sawa niue,na naomba nikwambie ukweli kabla hujaniua,nishawaambukiza ukimwi karibia ndugu zako wote,na kuna wengine tisini na moja,kuna karatasi za wanamme niliyowaambukiza ukimwi”
“Unasema nini?”
“Baba yako ndiyo alitaka haya yatokee”
“Malaya unasema nini Hafuan?Baba yangu ni mtumishi wa Mungu,mpaka nayeye umeamua kumuambukiza?”
“Ndio ivyo sasa wewe hujui kitu,fanya unavyo taka,na kitu kingine jina langu sio Hafuani naitwa Sonia Nickson Shayo”
Sonia aliongea kwa hasira na katika mazungumzo yake hakukua na tone la utani hata kidogo,
hiyo ilizidi kumkera zaidi Mzee Alex Mwandambo aliyekuwa mbele yake anamtizama kama chui aliyeona kitoweo amevimba kwa hasira,hapo hapo alishindwa kujizuia na kumtandika kofi.
“Rudia tena”
“Ndio ha…ta ukinitesa hauwezi kuubadili ukweli,nishakupa ukimwi tayari na muda mfupi utaenda kuungana na wenzako waliotangulia Alex”
Jasho lilizidi kumtoka Mzee Alex na kupandwa na mori za hasira maneno ya Sonia yalizidi kumchoma moyoni sababu aliona ndoto zake zote zimepeperuka,tamaa za mwili zilimponza na kujikuta amenasa kwa msichana mrembo aliyekuwa mbele yake.
Hakutaka kujiuliza mara mbili alirudi ndani ya gari na kutoka na bastola kisha kumsogelea Sonia.
“Hiki ndiko kinakutia Jeuri sio?”
Mzee Alex Mwanadambo alisema huku bastola yake akiwa ameikandamiza sehemu za siri za Sonia.
“Nakuuliza hiki kidude chako ndiyo kinakufanya uwe kiburi wewe Malaya?haya ndiyo malipo ya wema wangu na leo ndiyo mwisho wako”
Baada ya kuongea hayo Alex alichomoa magazine na kukagua risasi ndani ya chemba kama zinatosha,alikasirika zaidi baada ya kukuta kuna risasi moja peke yake.
Nia ya kuchukua bastola ilikuwa ni kumuua Sonia kisha yeye ajimalize pia.Kitendo cha kukuta risasi moja ndani ya bastola kilimchanganya akili yake,lakini alivyogeuza shingo yake nyuma aliona gari lake aina ya Prado linaunguruma bado.
Akawa amepata wazo jingine jipya,alirudi ndani ya gari na kulirudisha nyuma kwa kasi.
“Huwezi kupona leo”
Kitendo cha kurudisha gari nyuma kwa kasi kilimfanya Sonia aelewe nini maana ya kifo anachoenda kukabiliana nacho,aliogopa zaidi!
Hapo ndipo alipoanza kulia kwa uchungu, aliliona gari la Mzee Alex linarudi nyuma kwa kama umbali wa mita mia moja na mbili,na kuanza kusali sala yake ya mwisho, aliamini kuwa aliyokuwa akiyafanya hakupenda!licha ya yote alikuwa yupo tayari kwenda jehanam!
Mapigo ya moyo ya Mzee Alex yalimdunda sio masihala, bastola yake alikuwa ameikoki ipo pembeni ya gia na katika mahesabu yake alikuwa ni lazima amgonge Sonia na gari lake aliyekuwa mtini.
Kwa umbali aliokuwa yupo, aliamini kitendo anachoenda kukifanya kingemuondosha duniani.Aliweka gia namba moja na kuachia clachi kisha kulitoa gari kwa kasi, lilivyochanganya alishusha gia namba mbili likazidi kwenda kasi zaidi.
Gari lilikuwa katika mwendo wa ajabu likitimua mavumbi na alivyoukaribia mti alipofungwa Sonia aliyafumba macho yake,hazikupita hata sekunde mbili alisikia kishindo na kelele za sauti kisha ukimya kutawala.
Aliyafumbua macho yake taratibu na kuona damu juu ya kioo cha mbele huku kichwa cha Sonia kikiwa kimelala juu ya boneti la gari akiwa anavuja damu.Hakutaka kupoteza wakati, hapohapo alichukua bastola yake na kujiwekea kichwani huku akitetemeka mno,aliipenda sana familia yake hasa alipomkumbuka mke wake Latifah,alielewa ni jinsi gani ataenda kuteseka akiwa mjane,
lakini hakuwa na chaguo lingine,machozi yalimtoka na taratibu kidole chake kikiwa kinasogea kwenye kifyatulio kinachoitwa triga.
“Paaaaaaaaaaa”
Ubongo wa Mzee Alex ukawa umemwagika chini na damu kuruka kwenye vioo,fuvu lake la kichwa likawa limefumuliwa na risasi, huo ndiyo ukawa mwisho wa maisha yake duniani.
*****
Ilikuwa ni tarehe ishirini na moja mwezi wa kumi na mbili saa kumi na moja ya asubuhi siku ya Jumatano,Ubungo kulikuwa kuna hekaheka na tarehe hizo wachaga ndiyo husababisha vurugu wakigombania mabasi ya kwenda mikoani kwao kula siku kuu ya chrismass na mwaka mpya.
Kipindi cha mwezi wa kumi na mbili hata nauli zilikuwa ghali,Magari ya Dar express,Meridian,Msae yote yalikuwa yakijaza, hata pengine wachaga walikuwa wapo tayari kukalia makreti ili mradi tu waweze kufika mkoani Kilimanjaro, Moshi!
“Oyaaa Nickson,umepata siti?”
“Ndiyo George”
“Mimi nasepa,safari njema ndugu yangu,wasalimie bibi na babu waambie mimi kazi zimenibana nitakuja wiki ijayo”
“Poa poa aisee haina mbaya”
“Poa Meku safari njema Mzee,ukifika nivutie waya”
“Aminia aminia”Sauti ya kijana aliyekuwa nje chini ilisikika akiwa ana muaga mwenzake.
Basi la kampuni ya Meridian lilikuwa teyari limeanza kupiga honi kuashiria kuwa safari inatakiwa kuanza, na ilivyofika saa kumi na mbili juu ya alama mabasi yakawa yameruhusiwa kuanza safari,kila basi likaanza kuchomoka kwa kasi ubungo terminal.
Nickson alivuta pumzi na kutabasamu,alikuwa anatamani kufika mapema mkoani kwao Kilimanjaro.
Nickson alikuwa ni kijana wa miaka kati ya ishirini na tano mpaka na saba.Ni mwaka mmoja tu tangu apokee shahada yake ya sheria na alibahatika kuajiriwa na serikali katika mahakama ya kisutu, alikuwa ni kijana mzuri mweupe wa kichaga, aliyechanganyika na damu ya kirangi.
siku zote Nickson alitamani kuja kuoa mapema pindi tu atakapopata kazi, siku zote alitamani kupata familia bora na yenye misingi imara ya kidini.
Hata siku moja hakutaka kuja kuoa nje ya mkoa wake,alitamani kupata msichana wa kichaga na kitu kingine kilichokuwa kinampeleka Mkoani Kilimanjaro siyo kusalimia wazazi wake peke yake tu,bali kutafuta kigoli arudi naye mjini Dar es saalam,
hakutaka safari hiyo arudi peke yake,kama sio kurudi na msichana basi awe keshapata tayari.
Basi lilizidi kusonga mbele na lilivyofika kimara mwisho likawa limesimama kupakia abiria wengine.
“Kaka samahani hiyo siti namba ngapi?”
Sauti ya msichana mrefu ilimshtua Nickson aliyekuwa kwenye mawazo ya kupata kigoli.
“Ahaa hii siti?”
“Ndio”
Nickson akasimama kidogo na kuchungulia namba.
“E-6”
“Basi ndiyo hapa,samahani kaka?”
“Bila samahani”
“Ninaweza nikakaa dirishani?”
“Hakuna shaka”
Nickson akawa amempisha jirani yake kisha akapita dirishani.Kila mtu akawa kimnya na basi likaendelea na safari yake.Mpaka wanafika sehemu ya kula chakula cha Mchana inayoitwa ‘Liverpool’ hakuna hata mmoja aliyemuongelesha mwenzake.
Nusu saa baadaye safari ikaanza tena.
“Dada yangu tukifika Marangu niamshe”
“Ndiyo unaposhukia?”
“Hapana”
“Unashuka wapi kwani?”
“Mwika,Mwika, Kishingoni”
“Wewe mchaga wa Marangu mwika?”
“Ndio”
“Shimbonyi”
“Nashcha Mae”
“Mimi naitwa Rebeca”
“Nickson Shayo”
“Ukoo wakina shayo umesambaa kumbe,mimi Kimaro,ila mama yangu ni mchaga wa huko kwenu”
“Nafurahi kukufahamu aisee,nawewe unaenda kuhesabiwa sio?”
“Ha ha ha ha ha haaaaa”
Huo ndio ukawa mwazo wao wa kufahamiana.
Baadaye Nickson akawa amepitiwa na usingizi mzito na alipofika Marangu kama alivyotaka iwe, aliamshwa na jirani yake Rebeca.
Waliendeleza stori,hatimaye Nickson akawa anakaribia kufika safari yake,alianza kusimama na kuchukua mabegi yake yaliyokuwa juu sehemu maalumu.
“Konda Kishingoni hapo niache”
“Sogea sogea karibu kaka”
“poa”
Gari liliposimama Nickson akashuka na akapokelewa na wazazi wake ambao walikuwa wenye furaha kumuona mtoto wao.
Sasa unaweza kusoma hadithi za mtunzi kway insta@storyzakway
ITAENDELEA.
Labels:
HABARI & UDAKU,
LOVE & STORY
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment