Wakati maneno ya chini chini yakiwa yanaendelea kuhusu kupigwa kibuti
na mpenzi wake mpya Spicy kutoka Nigeria, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’
amefunguka na kusema wabongo wengi wanapenda wenzao waharibikiwe na
kuwataka kuacha kuwaziana mabaya.
Jide
amelazimika kutoa kauli hiyo baada ya maneno kuzagaa kuwa amepigana
kibuti na Mnigeria huyo ikiwa ni siku wiki chache baada ya kuandika
maneno yaliyomo kwenye... wimbo wa Rosella katika mtandao wa Instagram.
“Niko vizuri na Spicy, yale
maneno niliandika kwa ajili ya muziki, watu wanapenda kuona wenzao
wanaharibikiwa, kwanini wanakimbilia kuamini nina matatizo na Spicy na
hawafikirii kuhusu kazi yangu? Niwakaribishe waje kwenye show yangu ya
uzinduzi pale Lugalo Uwanja wa Gofu Ijumaa hii,” alisema Jide.
Lady Jaydee anayetamba na wimbo wa
Rosella alioshirikiana na h_art the band kutoka Kenya anatarajiwa
kuzindua albamu yake ya saba tarehe 31 ya mwezi huu.
0 comments:
Post a Comment