Friday, March 31, 2017
STORY: NILIFANYA MAPENZI NA MAITI 20 ILI NITAJIRIKE-24
ILIPOISHIA
Huo ndiyo ukaanza kuninyemelea. Mara ya kwanza, sikujali, ila baadaye, nilikuja kujuta kwa nini nilitaka utajiri.
SONGA NAYO
Kusema ukweli hakukuwa na kipindi nilichokuwa na furaha kama kipindi hicho, sikuamini kilichokuwa kikiendelea, maskini mimi, niliyeishi maisha ya ufukara mkubwa mkoani Morogoro, eti leo hii nilikuwa na...
mamilioni ndani ya chumba changu.
Maisha yalibadilika kabisa, nilifanya biashara kwa kujituma kiasi kwamba hakukuwa na mtu aliyehisi fedha zangu zilikuwa za kishirikina, nilitaka niwe tajiri mkubwa, mwenye biashara nyingi, niingize hata milioni mia moja kwa mwezi.
Nilijitahidi kufungua biashara mbalimbali tena zilizoniingizia fedha. Fedha zilimiminika, hakukuwa na aliyejua kilichokuwa kikiendelea zaidi ya Dickson tu ambaye alikuwa rafiki yangu wa karibu na ndiye aliyenipokea mara baada ya kufika Dar es Salaam.
Nilifanikiwa sana, nikaanza mipango ya kujenga nyumba yangu kubwa maeneo ya Goba huku nikinunua gari zuri kwa ajili ya kutembelea. Ndiyo hivyo, maisha yalibadilika na nilikuwa na kila sababu ya kutumbua pesa nilivyotaka.
Nakwambia kuhusu maisha yangu, nakwambia kwamba inawezekana kupata utajiri wa kishirikina lakini kamwe utajiri huo mwisho wake huwa mbaya mno. Niliwahi kuzungumza na watu wengi, najua nchi yetu imejaa maskini lakini kamwe usithubutu kupata utajiri kwa njia za kishirikina kwani huwa na gharama yake, shetani hatoi kitu pasipo kukuumiza, hatoi kitu pasipo kukupa masharti ambayo anajua kwamba utashindwa tu.
Wengi waliniona kama mwanamke anayejua kufanya biashara sana pasipo kujua nyuma ya maisha yale kulikuwa na nguvu kubwa ya kishetani. Kumbuka kwamba familia yangu ilikuwa maskini sana, wazazi wangu walihangaika kwenda shambani kila siku asubuhi, hivyo nilikuwa na kila sababu ya kuwasaidia.
Nilichokifanya baada ya siku kadhaa ni kurudi kijijini kwetu, sikupanda basi, nilitumia gari langu binafsi, Harrier nyeusi, mpya kabisa. Sikutaka kwenda kijijini moja kwa moja, nilitaka kupitia Ifakara kuonana na Mudi, yule mwanaume, utingo aliyenisaidia kiasi cha fedha kilichonifikisha Dar es Salaam, unamkumbuka?
Nilipofika Ifakara, nikaelekea mpaka katika kituo cha daladala. Wanaume wote wakabaki wakiniangalia kwa matamanio, nilikuwa mrembo mno, niliyenukia fedha kila nilipopita, walinitamani lakini kwa kuniangalia tu, hawakuona kama nilistahili kuwa nao.
“Unamuulizia Mudi anayeishi Mazobezobe?” aliniuliza mwanaume mmoja.
“Ndiyo! Yupo wapi?”
“Ametoka, ila msubiri, atarudi muda si mrefu, amekwenda Zilimpompa,” aliniambia kijana huyo, Zilimpompa ulikuwa mmoja wa mitaa hapo Ifakara.
Sikuwa na jinsi, sikutaka kuondoka mahali hapo, nakumbuka niliwahi kumwambia Mudi kwamba nilikuwa nikielekea Dar kutafuta utajiri na kuna siku ningekuwa tajiri, hakuwa akiamini, alinisaidia lakini najua aliona kwamba nakwenda Dar kupoteza muda, kujiuza na kufanya mambo mengine.
Leo hii nilirudi tena kwake, sikuwa Zakia yule maskini, nilikuwa Zakia mwenye pesa, niliyeendesha gari, niliyejipulizia manukato ya The Princess ambayo yalikuwa ni zaidi ya shilingi laki tano, nilikuwa na gari la kifahari, yaani kila nilichokuwa nacho, kilionesha kwamba nilikuwa na pesa.
Baada ya saa moja, huku nikiwa garini nimesinzia, mara nikasikia kioo cha gari langu kikigongwa, nilipoyafumbua macho yangu na kumwangalia mgongaji, alikuwa Mudi. Uso wake ulikuwa kwenye mshangao mkubwa, kwanza hakunijua mimi nilikuwa nani, nikakishusha kioo.
“Mudi, mambo vipi?” nilimsalimia huku nikimuonesha tabasamu pana.
“Poa,” alinijibu huku uso wake ukiwa kwenye maswali mengi.
“Unanikumbuka?”
“Hapana! Wewe unanijua?” alinijibu na kunitupia swali.
“Jamani mpenzi! Kweli hunikumbuki?” nilimuuliza huku nikimfungulia mlango na kumtaka aingie.
Akaingia, alionekana kujishtukia sana, alikuwa mchafu, mavazi yake yalichakaa sana. Humo, bado alikuwa na maswali mengi, mimi nilikuwa nani na kwa nini nilimuita ndani ya gari? Hapo ndipo nikamuweka wazi kwamba mimi nilikuwa Zakia, mwanamke yule wa miezi kadhaa iliyopita ambaye nilikuwa na safari ya kwenda Dar.
“Zakia! Ni wewe?” aliniuliza huku akinishangaa.
“Ndiyo! Nimeona nije kukusalimia,” nilimwambia.
“Imekuwaje tena?”
“Nini jamani?”
“Kuwa hivyo!”
“Hahaha! Nilikwambia nakwenda Dar kutafuta utajiri, si unaona nimeupata,” nilimwambia huku nikitoa tabasamu.
Alibaki akinishangaa, sikutaka kujali sana, nilimwambia kwamba siku hiyo nilikuwa mgeni wake, nilitaka kulala naye, kumbuka alinisaidia nauli, elfu hamsini, nilitaka nimlipe, siyo fedha bali kumpa mapenzi motomoto ambayo asingeweza kuyasahau maisha yake yote.
Tukaondoka na kuelekea katika hoteli moja iliyokuwepo hapo Ifakara, nikachukua chumba na kuingia chumbani, tulipofika, akakaa kitandani, akavua nguo, akaenda bafuni, ila aliporudi, nikashangaa sana, hakuwa yule Mudi ninayemfahamu, alibadilika na kuwa moja ya maiti niliyowahi kufanya nayo mapenzi, maiti iliyojaa damu ambayo nguo zake tu zilionesha kwamba alipata ajali. Nikashtuka sana!
“Kuna nini mpenzi?” aliniuliza swali hilo, hapohapo nikamuona akibadilika na kuwa Mudi.
Kiukweli nilichanganyikiwa sana, nilitetemeka mwili mzima na kuhisi mwili wangu kama umepigwa shoti fulani ya umeme. Mudi akanisogelea, akanitupa kitandani na kutulia juu yangu. Nilibaki nikimwangalia kwa macho yenye kurembua, tayari nilianza kuingia katika ulimwengu mwingine wa mahaba.
“Unanukia vizuri mpenzi wangu…” aliniambia, ghafla nikashtuka.
Maneno kama hayo niliambiwa na maiti ile ya kule makaburini kipindi alichotaka kufanya mapenzi na mimi. Maneno yaleyale ndiyo aliyoyazungumza Mudi, karibu kabisa na masikio yangu.
“Nashukuru!” nilijibu huku nikiachia tabasamu pana lenye hofu.
“Umetafuta sana utajiri, hakika utakuwa zaidi ya hapa, ninachokitaka ni wewe kuwa mpenzi wangu milele,” alisema Mudi.
Kiukweli alinichanganya sana, hapohapo nikamuona akitoka katika sura ya Mudi na kurudi katika sura ya moja ya maiti niliyowahi kufanya nayo mapenzi mochwari, hakika ilinitisha sana. Nikataka nijitoe pale kitandani, akanikandamiza zaidi. Nikahisi kifua kikianza kubana na pumzi kuanza kukata.
Je, Zakia atafanyaje na kwa nini alitokewa na maiti aliyowahi kufanyanayo mapenzi?
Labels:
LOVE & STORY
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment