MNENGUAJI wa kundi la Wasafi Classic (WCB), Moses Iyobo, amesema
hajawahi kufikiria kuwa mwimbaji kwakuwa ni kazi inayohitaji kutumia
akili nyingi tofauti na unenguaji.
Iyobo ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na aina yake ya
uchezaji, amesema ataendelea kubaki kuwa mnenguaji katika maisha yake
yote sambamba na kuwa mwalimu kwa... wenzake.
Alisema kazi ya kuimba inahitaji akili nyingi ili kufikia malengo hivyo ataendelea kubaki na kazi yake ya unenguaji.
“Nitabaki kuwa dansa maisha yangu yote, labda nitakachoongeza hapo ni
kuwa mwalimu na kuwafundisha wengine, unajua kuimba kunahitaji akili
nyingi ili ufanikiwe. Sasa kwa upande wangu sitaweza ni bora nibaki huku
huku ndio pananifaa zaidi,” alisema Iyobo ambaye ni mpenzi wa msanii
Aunt Ezekiel.
0 comments:
Post a Comment