Tuesday, March 28, 2017
NILIACHA USISTER NIKAWA MCHAWI 08
Akitoka pale tumpeleke njia panda ya siku zote ili tukamkabidhi kwa wahenga washughulike naye.” Yule mzee aliniangalia kwa macho yaliyojaa upendo, akaniuliza: ”Eti Mtiwati, upo tayari?” ENDELEA SASA… Nilitingisha kichwa kukubali. Palepale mkutano wote wa wachawi ukacheka kicheko cha kichawi. Najua hapa wengi watajiuliza kicheko cha kichawi kikoje?
Kwa kawaida mchawi anapocheka, wewe ambaye si mchawi kama utamsikia utajua ni mtu anacheka kinafiki, yaani anakilazimisha kicheko wakati sivyo inavyotakiwa. Au unaweza kujua anayecheka anaigiza lakini...
hacheki katika uhalisia. Mtu anapocheka pasipo uhalisia anajulikana tu. Basi, tuliondoka katika mazingira ambayo mimi sikuyafahamu hadi msibani, yaani nyumbani, mama akiwa mbele yangu aliniambia chochote atakachokuwa anakifanya mimi nimwigize, nikamjibu sawa kwa sauti ya chini sana.
Yule mwanamke mchawi aliyetoa wazo la kuja kwenda msibani naye akaniambia sitakiwi kujibana sauti wakati wa kuongea kwa sababu siwezi kusikika hata kama nitapiga mayowe. Nilimwelewa vizuri sana. Mama akiwa mbele yangu, wachawi wengine wote wakiwa nyuma yangu, tuliizunguka nyumba yetu kwa kurukaruka huku tukipiga makofi kwa juu, paa paa! Baada ya kuzunguka mara tatu.
Ulikuja kusimama mbele ya mlango mkubwa tukafanya kama foleni au mstari wa kutoka mlangoni kurudi nyuma. Mimi nilikuwa nyuma ya mama tangu tulipofika. Mama aliinua mikono juu kisha akaifumbia kwenye kifua kama mtu anayenyenyekea, mlango mkubwa ukafunguka wenyewe waaa! Nilianza kumwona shangazi, nikamwona mdogo wangu na kuwaona wengine wote waliolala sebuleni.
kumbukwe kwamba wakati huo nje hapakuwa na wanaume, wao walishaachana na kulala tanga nyumbani. Mama aligeuka na kutembea kuingia ndani na mimi nilifanya hivyo. Kumbe ndiyo staili kwani nilipogeuka tu niliona wengine wote walishageuka kabla yangu. Hapa namaanisha kwamba tuliingia ndani kwa kurudi kinyumenyume.
Kufika sebuleni, mama alianza kufuata watu na kuwatawazia huku akinonesha na mimi watu wa kuwafanyia kitendo hicho. Wachawi wengine pia kila mmoja alikuwa akimfanyia mtu wake, yaani kutawazia. Mimi niliamua kumfuata mdogo wangu mmoja, nikamtawazia, lakini huku nikiwa naogopa kwamba akiamka anaweza kupiga kelele lakini cha ajabu hakufanya hivyo.
Ilikuwa kama vurugu humu ndani, kwani mchawi yule alikuwa akimtawazia yule, mwingine kwa mwingine. Kazi hii ilifanyika kwa karibu dakika kumi na tano hivi. Mama ndiye aliyetangulia kutoka nje, nikafuatia na wengine wakaja pia. Hapo nje tulitengeneza mduara wa wachawi kumi na sita. Hapo labda niseme kwamba, hata tuliyoingia ndani ni kumi na sita. Baada ya mduara, mama alianzisha wimbo.
Hadi leo hii sijui ule wimbo ulikuwa wa kikabila au la! Lakini ulikuwa unasema hivi: “Mtekete mtekete, kambila mugwai, nanyane mitime. Mitime kambila mugwai.” Watu wote waliitikia hivyohivyo na kupiga makofi huku tukizunguka kucheza mduara kwa kuzunguka na makofi juu. Lakini nilijiuliza, vile tulivyokuwa tukifanya ni nini? Yaani itatufaidia nini sisi wachawi? Je, kama tusipoamua kufanya vile na tukawa tumelala hasara yake ni nini? Nilikosa majibu, lakini pia sikutaka kumuuliza mtu, nikasema moyoni kwamba mambo yote nitayajua siku zinavyozidi kusonga mbele.
Baada ya mchezo huo, mama alisimama, nikasimama nyuma yake, akanishika mkono. Kufumba na kufumbua tulikuwa njia panda. Lakini hapo tulikuta wachawi wengine kibao ambao walikuwa wakicheza michezo ya kichawi. Unaweza kusema walikuwa wakifanya vituko kwa jinsi walivyokuwa wakifanya. Tulijiunga nao, wachawi wote tukawa tunacheza huku wapiga ngoma wakiwa katikati. Mara mzee mmoja miongoni mwa tuliowakuta akatuliza ngoma kwa kuinua mkono juu. Ngoma nazo zikawa zinatulia polepole mpaka zikasimama kabisa, yule mzee akasema kwa hasira: “Leo wenye madeni wote wasimame huku pembeni.
Tunataka kujua watalipalipaje? Kwani ni muda mrefu sana umepita.” Wachawi kama kumi hivi walikwenda kusimama upande ule uliosemwa. Miongoni mwa wale waliotoka, alikuwepo bibi, wengine ni wale wachawi tuliowakuta. Awali sikushangaa bibi kutoka kwa sababu sikujua walikuwa wakidaiwa nini, lakini kilichofuata nilishangaa sana: “Nyie mmevuliwa sana, lazima leo kila mmoja aseme atakavyolipa. Mmekula nyama za wenzenu halafu kwenye zamu yenu mnakuwa wagumu, haiwezekani hata kidogo.” Ndipo nikajua kumbe bibi anadaiwa nyama.
Nilijua ni nyama za watu kwani simulizi hiyo kwamba wachawi wanakula nyama za binadamu wenzao ilikuwa inajulikana kwa hiyo isingekuwa rahisi nidhani ni nyama ya ng’ombe au kuku. “Wewe bibi Mtiwati…” Kama nilivyokwisha sema, Mtiwati ni mimi kwa jina walilonipachika wachawi kule porini: Je, bibi kizee huyo mchawi anamtaja Benadeta? Fuatilia mkasa huu Ijumaa ijayo.
“Mbona mama Mtiwati ameshalipa deni, mumewe mzimamzima amemtoa, wewe lini na atakuwa nani?” Bibi aliangazaangaza macho huku na kule kisha akasema: “Mwezi huu hauwezi kupita.” “Mwezi huu hauwezi kupita. Sawa tumekusikia. Hata atakuwa nani?” Nilimwona bibi akigeukageuka kunitafuta niliposimama, nikashangaa ni kwa nini bibi anitupie macho mimi wakati nimeshakuwa mchawi mwenzao? Je, anataka kunitaja nini?” nilijiuliza hivyo huku miguu ikinichezacheza kwa wasiwasi. Je, bibi kizee huyo mchawi anamtaja Benadeta?
Labels:
HABARI & UDAKU,
LOVE & STORY
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment