Thursday, March 30, 2017
NAY WA MITEGO: TUSIPO ANGALIA SIASA ITATUZIDI NGUVU MZIKI UPOTEE KAMA BONGO MOVIE
Nay wa Mitego amedai kuwa kama wasanii wa Bongo Flava wasiposimama kidete kuupigania muziki wao, kuna hatari ukapotezwa na siasa. Amedai kuwa siku za hivi karibuni mashabiki wamekuwa wakifuatilia zaidi mambo ya siasa kuliko wanavyofuatilia muziki, na anasema hiyo ni hatari.
“Watu walikuwa wanasikiliza siasa zaidi kwamba leo nini kinaendelea, leo kiongozi gani ameongea kitu fulani, nafikiri sasa ni time ya sisi kupambana kuurudisha muziki wetu kwenye line, kuurudisha muziki wetu watu...
wausikilize muziki, siasa na vitu vingine ambavyo vinaendelea, skendo, kiki, viwe vya baadaye,” rapper huyo amemuambia mtangazaji wa Jembe FM, JJ.
Nay ameonya kuwa kama wasanii wa muziki wasipokomaa, wanaweza kujikuta wakipumulia mashine kama wenzao wa bongo movie ambao soko lao linazidi kuporomoka.
Kwa upande mwingine Nay amedai kuwa wimbo wake Wapo umefanya muziki uanze kusikilizwa tena. Ijumaa hii rapper huyo anakutana na Rais Dkt John Magufuli baada ya kuitwa Ikulu kufuatia wimbo wake Wapo uliokosoa serikali.
Dkt Magufuli aliamrisha kuachiwa huru kwa rapper huyo na kudai wimbo wake Wapo uendelee kuchezwa redioni.
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment