Msanii Baraka
The Prince anayetamba na wimbo wake wa ‘Niache Niende’ amesema wakati
wake ukifika naye atajiingiza katika mambo ya filamu nchini kama
alivyokuwa Hemed PHD.
Msanii huyo ameelezea hisia zake kwa
kile anachokiamini kwa kusema yupo katika harakati za kujenga ‘brandy’
yake ya muziki ili itambulike vizuri katika soko huku akidai alishawahi...
kufuatwa na director mkongwe katika tasnia ya filamu maarufu kwa jina
la Mtitu.
“Nilishafuatwa kabisa na
yule ‘director’ Mtitu aliyemtoa Kanumba alikuwa anataka tufanye ‘series’
mimi niwe 'starling' na Irene Uwoya lakini kwa kipindi kile sikuwa
‘ready’ kuingia kwenye mambo ya ‘movie’ lakini bado sijawa ready
kwasasa hivi kwasababu bado najenga Brandy yangu”. Alisema Baraka
Aidha Baraka amesema endapo siku
watanzania watasikia msanii huyo ameingia rasmi huko basi wajue itakuwa
moto wa kuotea mbali kwa kuwa hata video zake za muziki anazozitengeneza
huwa anaigiza sana.
Kwa upande mwingine 'hitmaker' huyo
amesema hakuna ukweli wowote unaohusiana baina ya maisha yake na
mashairi anayoyatumia katika wimbo zake huku akisisitiza kuwa anaimba
kutokana na vitu vinavyotokea kwenye jamii inayomzunguka.
0 comments:
Post a Comment