Msanii Khalid Chokoraa aliyekuwa anafanya vizuri katika miondoko ya dansi amekanusha zile tetesi ya yeye kufeli muziki wa singeli na kusema hakuna ukweli katika hilo kwa sababu kazi zake mpaka sasa zimepata mapokezi mazuri pamoja na ‘airtime’.
Akiongea kupitia kipindi cha eNewz
Chokoraa amesema hawezi kushangazwa na hayo maneno kwa kuwa kila kitu ni
mipango huku akisisitizia watu wawe... na subira watamuelewa anachokifanya
japokuwa itachukua muda mrefu.
“Mimi malengo yangu yanaenda
vizuri kwa sababu kila kitu ni mipango tu, huwezi kuwa na 10 bila ya
kuanza moja kwa hiyo tunaenda vizuri kwenye muziki wa singeli,
nimeshaachia nyimbo mbili mpaka sasa, ya kwanza inaitwa ‘Baba mwenye
nyumba’ na ya pili nimefanya na Kalala Junior. Tunajiita watoto wa nje
ya ndoa”. Alisema Chokoraa
Pamoja na hayo msanii huyo amesema yeye
amezaliwa ndani ya ndoa ila ameamua kutumia jina la watoto wa nje ya
ndoa kama mwamvuli kwa watu wanaomzunguka ambao hawajapatikana katika
mchakato wa halali.
Kwa upande mwingine Chokoraa amesema
hana mpango wa kutoa albam kama wasanii wengine ila yeye ataendelea na
ule utamaduni wa kuachia ‘ngoma’ kisha kufanya ‘show’ kwa madai kuwa
albam hazilipi
0 comments:
Post a Comment