Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa
Mitego ameitwa Ikulu jana jioni kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais
John Magufuli.
Nay alipata mwaliko huo ikiwa ni sasa chache baada ya kuachiwa huru na Jeshi la Polisi lililokuwa likimshikilia tangu juzi, Katika mahojiano yake na kituo cha Televisheni cha Azam Two, Nay
alikiri kupata mwaliko huo na kueleza kuwa... ataitumia vyema nafasi hiyo
kumuelezea Rais Magufuli hali halisi ya maisha ya Watanzania.
“Nimepokea mwaliko bado nafikiria nini cha kuongea naye endapo nitapata
hiyo nafasi ya kuzungumza naye, nadhani itakuwa nafasi nzuri ya
kumweleza vile ambavyo Watanzania sisi tunaishi mtaani,”alisema.
Nay alikamatwa na polisi juzi mkoani Morogoro na kusafirishwa hadi Dar
es Salaam kwa kile kilichodaiwa kutunga wimbo wenye maudhui
yanayoikashifu Serikali.
Mapema jana mjini Dodoma, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Dk Harrison Mwakyembe alisema Rais Magufuli ameagiza msanii huyo aachiwe
huru na wimbo wake uendelee kuchezwa na kusambazwa.
0 comments:
Post a Comment