Mwanamuziki wa Kike kutoka nchini
Marekani Rihanna anatarajia kupokea tuzo kutoka kwenye shule ya mitindo
maarufu inayojulikana kwa jina la “The Parsons School of Design”.
Hii ni Tuzo nyingine kwa mwanamuziki huyo, mara baada ya muda mfupi kupokea heshima kubwa ya kutajwa kama Harvard’s Humanitarian of the Year
ikiwa ni heshima ambayo imemweka kwenye ligi moja...
na katibu mkuu wa
zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan na muigizaji James Earl Jones.
Heshima hiyo kutoka Harvard ilitokana na
shughuli zake za kusaidia elimu katika nchi maskini kupitia taasisi yake
ya Clara and Lionel Foundation.
Kwa mujibu wa Billboard
imeripoti kuwa, Kwa kipindi cha nyuma chuo hicho cha sanaa na ubunifu
kilitoa tuzo hiyo kwa Donna Karan ambae ni mwanzilishi wa kampuni
inayojihusisha na mitindo DKNY yani, Donna Karan New York.
Imeelezwa kuwa tuzo hiyo ni maalum kwa
ajili ya watu ambao wanawawezesha na kuwasaidia wasichana wadogo. Na
chuo cha parsons kimempa heshima hiyo Rihanna kutokana na kazi zake za
muziki, wanamitindo, na uhisani wake.
Na
septemba mwaka huu tutegemee kumuona Rihanna pamoja na kampeni yake ya
clara lionel kwenye tamasha la diamond ball kwaajili ya kusaidia
kuchaingia fedha za afya na elimu duniani kote.
0 comments:
Post a Comment