Meneja wa Msanii Snura, HK amesema yeye pamoja na msanii wake hawana
'bifu' na Shilole huku akidai wapo tayari hata kufanya naye kazi ya
pamoja endapo atakuwa anahitaji katika hilo.
Hayo yamekuja baada ya tetesi za muda
mrefu zikiwahusisha wadada hao wawili kwa kile kilichowaaminisha
mashabiki katika nyimbo zao kujawa mafumbo huku wengine...
wakiyatafsiri
ndivyo sivyo.
"Mimi nafikiri bifu ya
Shilole na Snura zinatengenezwa na mashabiki wenyewe kutokana hawa wote
walitoka kwenye bongo muvi wakaja kwenye bongo fleva, alianza Shilole
akaja Snura. Wote wakatusua katika kipindi kimoja, yule ametoa 'Paka wa
Baa' ina-hit kule Snura anatoa 'Majanga' nayo ina-hit kwa hiyo
wakakutana katika 'game' watu wakawa wanafananisha kulingana na
walipotoka lakini siyo wana bifu mpaka inafikia hatua hawaongei siyo
kweli". Alisema HK katika kipindi cha eNewz kinachorushwa na EATV.
Aidha meneja huyo amesema ameshawahi kuwaona mara nyingi wanadada hao wakiwa pamoja wanasalimiana na kuongea.
Kwa upande mwingine HK amesema yupo
tayari yeye na msanii wake kufanya kazi pamoja na Shilole endapo
atakubali muda wowote milango ipo wazi katika suala hilo.
0 comments:
Post a Comment