Ikiwa ni miezi michache sasa imepita toka tusikie wimbo wa ‘I’ m Sorry JK’
umefungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwa kile alichosema
Nikki Mbishi kuwa aliambiwa hauko kwenye maadili, ingawa Baraza la Sanaa
lenyewe halikuthibitisha kuufungia wimbo huo lakini walichothibitisha
ni kumuita Nikki Mbishi na kuongea nae.
Katika ngoma hiyo, Nikki alijaribu
kuonesha jinsi ambavyo alikosea kuukosoa utawala wa awamu ya nne, huku
akikutana na hali ngumu zaidi katika...
utawala wa awamu ya tano, ambapo
anafikisha ujumbe unaomaanisha kuwa utawala wa Rais Mstaafu Jakaya
Kikwete ulikuwa bora kuliko wa sasa.
Anyway, Leo kupitia ukurasa wake wa
twitter baada ya kusikia kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia Waziri wa Habari, Sanaa, Tamaduni na Michezo Dkt.
Harrison Mwakyembe kuruhusu wimbo wa Nay wa Mitego uendelee kuchezwa na
pia kuusifia kuwa mzuri, Nikki ameuliza vipi kuhusu wimbo wake wa ‘I’ m Sorry JK’.
Ujumbe huo ulisome hivi.. “Vipi kuhusu “I’m Sorry JK” ? Ina maana ina maneno makali au mabaya yasiyosikilizika au niaje?”
(Kwa ufupi) Wapo ni
ngoma mpya ya Nay wa Mitego ambayo inadaiwa kuwa na uchochezi na leo
asubuhi kupitia Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) lilitoa taarifa ya
kuufungia wimbo huo ‘Wapo’ wa rapa Nay wa Mitego kwa madai wimbo huyo
hauna maadili.
Ikiwa ni masaa machache kupita, Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe, alidai
kuwa Rais Dkt John Magufuli ameagiza kuachiwa huru kwa Nay wa Mitego.
Jambo lililowashangaza wengi baada ya kauli hii kutoka kwa Rais.. ‘Nay
auboreshe zaidi wimbo huo kwakuwa umegusa masuala muhimu’.
“Yaani asiondoe kitu chochote, ila aongeze kwasababu unaelezea changamoto zilizopo kwenye jamii halafu wanaitikia watu ‘wapoo”. Kwa mujibu wa Dkt Harrison Mwakyembe kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma leo.
0 comments:
Post a Comment