March 26, 2017 kupitia mtandao wa Instagram Meneja wa msanii Diamond
Platnumz, Babu Tale aliandika kuhusu Wizara ya Maliasili na Utalii
kushindwa kuwatumia watu maarufu nchini kuutangaza utalii
wa Tanzania akiwataja mwanasoka Mbwana Samata na mwanamuziki Diamond
Platnumz kati ya watu wanaofanya vizuri kimataifa lakini hawapewi dili
hizo.
Alipotafutwa Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne
Maghembealisema>>Wasanii wetu wenye majina makubwa watangaze tu
Tanzania. Tanzania ni nchi yao sio lazima mpaka...
waambiwe waje tukae
pamoja tupange mikakati na tuangalie ni kitu gani anaweza kufanya na
watusaidie kutangaza utalii wetu.”
Baada ya Babu Tale kusikia majibu ya Waziri Maliasili na
Utalii Prof. Jumanne Maghembe ameamua kutumia ukurasa wake wa instagram
kuandika anachofikiria au namna alivyomuelewa Waziri.
“Duh hapa sijui mimi mshamba au sijamuelewa vizuri Mh Waziri kuhusu
kuitangaza Tanzania mimi kwa akili yangu fupi naona watu wa nchi jirani
wanatafuta wasanii watanzania kutangaza nchi zao hapa kwetu tunaambiwa
tuombe ili tutoe msaada mh sasa hela ya wizara inaenda wapi???? – Babu Tale.
“Cha ajabu unaweza ukaambiwa uitangaze nchi halafu utapelekwa mbugani
bure duh. Ninachojua kila sekta inamfuko sasa hili eneo la utalii mfuko
upo wapi mimi naendelea kuuliza mfuko wa kuitangaza Tanzania kwa nia
nzuri na mazuri yaliyopo umewekwa wapi??>> – Babu Tale.
“Leo wasanii wengi wanakimbilia hata kufanya video zao nje ya nchi
sababu ukitamani kufanya kitu nchini inakuwa kama mtu anakukomoa
usifanye. Hvi Samatta anavyofunga magoli wangewaza kumvalisha bendera ya
tanzania nguo yake ya ndani pale anapofunga goli avue watu waone
duniani kuna nchi inaitwa Tanzania ingekuwa je?>> – Babu Tale.
“Sina nia mbaya ila tuamke kweli kuitangaza nchi yetu na sio wahusika
waifuate sekta husika wakati kila sekta inakitengo cha matangazo na
wanajua nani wakupewa jukumu #mtazamochanya#Tanzania #” >> – Babu
Tale.
Thursday, March 30, 2017
MENEJA WA DIAMOND PLATNUMZ AMKABA KOO WAZIRI WA UTALII JUU YA PESA ZA WIZARA YA MATANGAZO
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment