Baada ya kuwepo tetesi za wasanii wa kike kubaniana nafasi, Maua Sama
amefunguka na kudai hayo ni maneno ambayo yapo na hayakwepeki kwa sababu
watu wamekariri kwa kusikia zaidi kuliko kufanya utafiti.
Maua
amesema kuwa tetesi hizo hazina tofauti na zile ambazo wanawake husema
wanaume wote ni sawa na kuongeza kwamba yeye hajawahi kukutana na
changamoto hizo kwa kuwa kila alipoenda kuhitaji ushirikiano na...
watoto
wa kike alipatiwa.
Aidha Sama ameongeza kuwa lisemwalo
linawezekana likawepo lakini kwa vile yeye si muathirika wa matendo hayo
ndiyo maana anashindwa kuweka bayana.
“Inawezekana kweli wanawake
hatupendani, siwezi kumuongelea kila mmoja mimi binafsi sijawahi kupata
changamoto hiyo na hata baadhi ya wasanii waliohitaji msaada wangu huwa
wanaupata haraka kwa sababu mimi ni mtu wa upendo ndiyo maana nadhani na
mimi huwa wananirudishia fadhila” – Maua Sama.
Maua ameongeza kuwa watu wengi
wanashindwa kumkariri katika nyimbo zake kwa kuwa tayari ni utaratibu
aliokwisha kuuweka tangu mwanzo wa kubadilisha ladha ya muziki ili
aendelee kusimama imara katika muziki.
0 comments:
Post a Comment