Msanii Nikki wa Pili kutoka katika kampuni ya Weusi amelitaka Baraza la
Sanaa Tanzania (BASATA) kufanya mpango kuwaita wasanii kwa ujumla ili
wakae pamoja waweze kuwaweka sawa juu ya neno "maadili" linalotumiwa
kama fimbo ya kuwachapa 'wasanii'.
Ametoa neno hilo leo wakati wakitambulisha wimbo wao mpya unaoitwa 'Ya Kulevya'
kupitia kipindi cha Planet Bongo ya EA Radio amesema wamekuwa katika
njia panda baada ya kushindwa kuelewa... neno hilo linavyotumika huku
akiwatoa wasiwasi wadau wa muziki na mashabiki zao kuwa wimbo huo mpya
hauna maana ya vitu vinavyoendelea nchini kwasasa.
"Wimbo wetu wa 'Ya kulevya'
huu ni wimbo wa mapenzi unaozungumza juu ya mwanaume aliyependwa sana na
mkewe na familia yake, upendo ukamlevya akaanza kujisahau na kula bata
na mwishowe kuharibu familia, tunasikitishwa na watu wanaojaribu
kubadili maana hii, imekuwa kawaida kwa msanii kutumia maneno au misemo
iliyoko katika jamii wakati huo kwani hata matangazo ya biashara,
'Comedy' hufanya hivyo ili kuwavutia wateja wao".
Alisema Nikki wa Pili Vile vile msanii huyo alisisitiza kwa kusema kuwa kabla ya kutoa kazi hiyo imekaguliwa na chombo cha maudhui ya sanaa
0 comments:
Post a Comment