Sunday, April 2, 2017
STORY: PENZI LA DADA (SEHEMU YA SABA) 07
Coleen aliniangalia kwa huruma kisha akasema "je ulishawahi kufanya kitu
kama hicho hpo kabla"??? nikajibu hapana leo ndio mara ya kwanza akauliza tena "ulikua unafikiria nn kabla haujapatwa na hisia zote hizo"!? nikamjibu Tayna!
oooh! ndio mana kwahiyo nadhani ulikua unafikiria ingekuaje kama mngekua ktk fungate lenu si ndio" Coleen siku zote alijua kuotea nnachofikiria alikua sahihi kabisa hicho ndicho nilikua nafikiria basi akanipa moyo na kuniambia...
usimfikirie sana kwani kikubwa unachoweza kufanya ss ni kumuombea apumzike kwa amani huko alipo, najua sana ilimpenda Tayna ila mungu kampenda zaid na ss hatuna budi kukubali hilo! akanisimulia wakati mume wake alivyofariki kama sio watoto wak wadogo wawili basi alikua hatamani tena kuishi kwahyo anajua yote nnayopitia.
Basi stori ghafla zilianza kubadilka hatimaye tukajikuta tupo ktk stori za kuchekesha wote tukiwa tunacheka na kufurahi kutokana na stori za shule tuliongelea
hadi kuhusu rafiki yake mmoja ambaye aliyeniunganisha nae hadi tukawa wote kisha
tukafumwa tukifanya mapenzi na mama yake! nilimsimulia jinsi nilivyokimbia na chupi tu na kuruka kutoka dirishani akikumbuka stori hyo
huwa anacheka sana.
Turifurahi hadi jua likachomoza bila kulala tena na ilikua tumepanga asubuhi na mapema kwenda kutembelea jiji la Lio de jeneiro hadi lilipo sanamu kubwa la YESU! ambalo ni kivutio kikubwa jijini hapo likiwa limetengenezwa kwa ustadi mkubwa na wa kuvutia sana basi tulikunywa chai kisha tukatoka nje kuchukua gari ambayo
tuliandaliwa na hyo hotel kwa ajili ya matembezi yetu ndani ya mji.
Basi tulipanda gari na kuanza safari ya kupitia sehemu mbalimbali za mji wa lio de jeneiro kwanza tukianzia ktk Zoo moja kubwa sana ktk jiji hilo kama isifikavyo Brazil na America kusini yote kua na nyoka wa kubwa sana basi hapo napo tulibahatika kumuona nyoka mwenye urefu wa futi 6 Coleen alikua muoga wa nyoka sana baada ya kumuona yule nyoka alishindwa kumuangalia na kukimbilia nilipo na kunikumbatia basi nikamshika hadi, tulipotoka hapo ndipo
akaniachia!
Majira ya saa 5 asubuhi tulifika ktk academia moja ya mpira ambayo watoto wa
kibrazili wanaonyesha ujuzi wa kuuchezea mpira. tuliburudika kwa muda watoto wakionyesha kipaji cha ajabu na kudhihilisha usemi kua mpira kweli kwao Brazil
basi hadi majira ya saa 7 mchana bado tulikua hapo tukaamua kuondoka na kutafta mahala tutakapokula chakula cha mchana.
Dereva anaetuendesha akachagua mgahawa mzuri kisha tukafika hapo na kuagiza chakula cha asili ya kibrazil kilichokua kinaitwa "veis" kilikua ni mchanganyiko wa viazi vya kuponda,nyama ya kusaga na ngano wote tulikula na kukifurahia chakula hicho baada ya kushiba na kulipa deni letu........ tukainuka kuanza safari ya kuelekea ktk sanamu la YESU dkk ishirini baadae tulikua tushafika lilipo sanamu Coleen alifurahi sana kuliko maelezo kila akicheka Coleen huwa kuna vishimo vinatokea usoni siku zote huwa napenda kumuangalia akicheka, basi nililizika kuona Coleen kaafurahi sana.
Tukapiga picha za ukumbusho na kupata historia kutoka kwa wahusika kisha saa moja jioni tukaanza safari ya kurudi hotelini huku mvua kubwa ikiwa inanyesha na radi zinapiga Katika vitu vyote Coleen anaogopaa sana Radi mda wote wakati tunalejea hotelini nilikua nimemkumbatia...........baada ya kufika hotelini tukaingia kwanza mgahawani na kula mlo wa usiku huku mda wote nikiwa nimemshika mkono Coleen kwani alikua anaogopa sana! baada ya kumaliza kula tukaanza safari ya kurudi chumbani ambako tulikaa tukiwa tunaangalia Tv!
Baada ya wote kuchoka tuliamua tulale, ila Coleen alishindwa kwa kuogopa radi ilibidi nihamie kitandani kwake ili kumtuliza..
Itaendelea....
Labels:
HABARI & UDAKU,
LOVE & STORY
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment