Msanii Msami amemchana AT na kumtaka
aboreshe kazi zake badala ya kulalamika kuwa kuna watu wanaobebwa huku
akimuonya kwamba wasanii anaowaita wacheza shoo wana maisha mazuri na
mafanikio makubwa kumzidi yeye.
Msami ameonesha kukerwa na kauli ya AT
iliyodai kuwa wanaobebwa kwenye muziki ni wale wanao ‘dance’ huku wakiwa
hawajui kuimba. Katika hatua nyingine msanii huyo ameongeza kwamba AT
hana...
ubora wowote kikazi ndiyo maana hawezi kuleta changamoto na wala
hajawai kufikiria kufanya naye kazi, huku akimkumbusha kuwa hao
anaowaita wacheza show huwa anawatafuta kipindi anapokuwa anawahitaji
kikazi.
Kwenye Interview na eNewz wiki hii, Msami amedai
“AT anaongea tu kawa sababu hao dancers anaowasema yeye wana maisha
nazuri kuliko yeye, wana fanbase kubwa na wanafanya maendeleo kibao kwa
kutumia vipaji vyao. Lakini cha ajabu sisi ambao ni madancers watu
wanapenda muziki wetu na tukipanda stejini watu wana enjoy, kwa kuwa
unawaimbia na bado unawaburudisha .
Aliongeza, “Lakini hapo hapo bado alikuwa ananipigiaga simu nimtafutie wacheza show akiwa na kazi”
Mbali na hilo Msami ameongeza kwa
kuwataja wasanii kutoka kundi la Makomando kwamba ni wabunifu lakini
wakati huo huo wana uwezo mkubwa wa kuimba kuliko AT hivyo inampasa
kuwaheshimu hao anawaita ma -‘dancers’ kwa sababu Mungu pekee ndiye
ameamua wafike walipofikia.
Msamii anayetamba na ngoma mpya ya ‘So Fine‘
amesema yeye kabla ya kuanza kuimba alikuwa mcheza show na mafanikio
makubwa aliyapata kupitia kazi hiyo kama kununua gari lake la kwanza,
kujenga nyumba na kuhudumia familia yake hivyo kumtaka AT asizungumze
mambo asiyoyajua.
0 comments:
Post a Comment