Msanii wa muziki wa asili nchini Mrisho
Mpoto amewataadharisha watu kwa wale wanaopenda kugawa simu zao kwa watu
wengine huku wakiwaruhusu wapige, waingize vocha zao, waandike ujumbe
mfupi au wafanyie chochote kile bila ya mwenye simu kujua anachofanya na
huenda kinaweza kuhatarisha maisha ya wengine na yako pia.
Mtunzi huyo mahiri ya mashairi ya
Kiswahili ambaye aliwahi kutajwa na vyombo vya habari kutaka kugombea
ubunge katika uchaguzi iliopita wa mwaka 2015, amekuwa akichambua...
baadhi
ya matukio yanatokea nchini.
Alhamisi hii ameibuka na kuwataadharisha
watu kwa kutumia hadithi fupi ya Dereva Taxi, Bwana Juma juu ya matumizi
sahii ya kifaa hicho (Simu).
(Instagram post)
“Bwana Juma ni Dereva Taxi maeneo ya
Mwananyamala kwa kopa siku moja alifuatwa na jamaa mmoja ampeleke sinza
kwenye nyumba Fulani ya wageni .Walipofika pale Yule jamaa akasema
ameishiwa chaji kwenye simu yake akamuomba juma simu yake atumie kupiga
ili awasiliane na mwenyeji wake pale nyumba ya wageni , simu ya juma
haikuwa na hela .
Walipokaribia ile nyumba ya wageni
Yule jamaa akaomba kushuka anunue vocha atie kwenye simu ya juma halafu
awasiliane na mwenyeji wake , juma akakubali , jamaa akanunua vocha
akaingiza kwenye simu ya juma halafu akawasiliana na mwenyeji wake
.Walipofika sehemu husika jamaa akashuka akaingia ndani ya nyumba
kumfata mwenyeji wake ambaye alikuwa mwanamke huku juma akiwa
ameshaondoka zake kwa sababu alikuwa ameshakamilisha shuguli yake.
Siku iliyofuata iligundulika maiti ya
mwanamke ndani ya kile chumba , simu ilikuwa mezani na vitu vingine
vyote hakukuonyesha kama kulikuwa na vurugu au mikiki yoyote ile
.Uchunguzi wa awali ulifanyika pale chumbani kwenye kifaa cha kuwekea
taka na simu ya Yule mwanamke , hapo mwili wake ulikuwa chumba cha maiti
ukifanyiwa uchunguzi pia .Kwenye kifaa cha kuwekea taka iligundulika
vocha moja iliyotumika , ilipofuatiliwa iligundulika iliwekwa kwenye
simu ya juma ikatumiwa kumpigia huyu mwanamke aliyekutwa na mauti.
Dereva wa taxi akatafutwa akapatikana ,
kukaguliwa gari yake ikagundulika vocha nyingine ya simu iliyotumika
katika moja ya milango ya taxi hiyo .Bwana Juma yuko Ndani kwa mashtaka
ya mauaji na uchunguzi unaendelea kufanyika mpaka hapo itakapokuja
kujiridhisha si yeye aliyefanya tukio hilo.
Inawezekana wewe ukawa ni bwana juma
ajaye , unayependa kugawa simu yako tu kwa watu wapige , watu waingize
vocha zao , watu waandike ujumbe mfupi au wafanyie chochote kile bila
kujua unachofanya kinaweza kuhatarisha maisha ya wengine na yako pia
.Simu na namba yake ni mali yako imesajiliwa kwa jina lako , wakati
unasajili uliingia mkataba wa kutumia kifaa hicho bila kuvunja sheria
zozote za nchi muda wote .Kina juma wako wengi , tazama usiwe mmoja
wao” aliandika msanii huyo Instagram.
Mwanamashairi huyo mbioni kuachia ngoma yake mpya.
0 comments:
Post a Comment