tafiti zilizofanywa na jarida la new england journal of medicine nchini
uingereza limegundua kwamba zaidi ya watu milioni moja na laki sita
wanauawa na na ulaji wa chumvi kila mwaka, kifo ni hatua ya mwisho ya
madhara ya chumvi lakini kuna madhara mengi sana yasababishwao na chumvi
kabla ya kifo.
kitaalamu chumvi ni kompaundi au mchanganyiko wa element za sodium
chloride, kemikali hii hutumika kuhifadhi chakula na kuleta ladha ya
chakula, kemikali hii huweka... kiwango cha maji mwilini sawa na kusaidia
utumaji wa taarifa kwenye mishipa ya fahamu, husaidia kuhifadhi maji
mwilini, ni muhimu kwenye damu ya mwili,kutengeneza tindikali kwa ajili
ya mmengenyo wa chakula tumboni, hata dripi za maji tunazopewa
mahospitalini hua zina chumvi.
maisha ya kisasa na vyakula viulivyopo vinawafanya watu kula chumvi
nyingi sana kuliko zamani, hii husababisha madhara makubwa ambayo
hayatibiki kirahisi.
kiafya mtu anatakiwa ale chakula chenye chumvi inayosikika kwa mbali
sana na asiongeze chumvi chakula kinapokua mezani, hii ni sawa na gramu
1.5 mpaka 2.3 kwa siku, hii ni sawa na kijiko kimoja cha chakula kwa
siku nzima.
ulaji mkubwa wa chumvi kwa wakati mmoja husababisha kuishiwa maji kwa
seli, hii huleta kuchanganyikiwa, degedege, kupoteza fahamu na kifo
lakini pia uwepo wa chumvi kidogo sana kwenye damu husababisha kuvimba
kwa seli, kuchanganyikiwa,kupoteza fahamu na kufa..hii hutokana na
unywaji mkubwa wa maji kupitiliza kiasi kwa wakati mmoja.
kimsingi vyakula vingi tunavyokula vina chumvi ya kutosha ambayo
inatosha kabisa kuendesha mwili wetu bila kuongeza chumvi nyingine ya
ziada, vyakula hivyo ni kama vitunguu,malimao,maji ya
kunywa,viazi,ngano,nyanya,maboga,caroti, spinachi, kabechi,mapera,
zabibu,epo,karanga,mayai, maziwa na vingine vingi
yafuatayo ni madhara ya ulaji wa chumvi nyingi ambayo yanaweza kua ya muda mrefu au ya muda mfupi.
yafuatayo ni madhara ya muda mrefu wa kula chumvi nyingi kwenye chakula...
presha ya damu; chumvi ina tabia ya kuzuia maji kutoka nje ya
mwili kupitia mkojo, lakini pia kuna ushahidi kwamba kupunguza ulaji wa
chumvi kwa wagonjwa wa presha hupunguza presha kwa wagonjwa wa presha.
kansa ya tumbo; utafiti umeonyesha kwamba nchi ambazo kuna ulaji
mkibwa sana wa chumvi kama japani kuna wagonjwa wengi sana wa kansa ya
tumbo la chakula ukilinganisha na nchi ambazo hazina ulaji mkubwa wa
chumvi kama uingereza.
ugonjwa wa moyo; chumvi husababisha kuvimba kwa moyo na kuufanya
kua mkubwa kitaalamu kama left ventricular hypertrophy, hii husababisha
moyo kushindwa kusukuma damu kama unavyotakiwa kufanya kazi.
magonjwa ya figo; kupanda kwa presha ya damu husukuma damu nyingi
sana kwenye mishipa ya damu, hii huharibu figo na kuifanya kushindwa
kutoa maji mwilini lakini pia viungo muhimu kama macho na mishipa ya
damu huharibika.
addiction; ulaji mkubwa wa chumvi humfanya mlaji kuendelea
kupenda vyakula vyenye chumvi nyingi sana na kushindwa kabisa kuvumilia
kula vyakula vyenye chumvi kidogo...hii hizidi kuathiri mwili na
kuusababishia matatizo makubwa zaidi.
kiharusi; huu ni ugonjwa wa kupooza unaosababishwa na kuziba kwa
mishipa ya damu ya kwenye ubongo kutokana na mafuta au kuvujia kwa damu,
kwa ulaji wa chumvi nyingi huongeza presha ya damu na kupasua mishipa
midogo ya kichwa na kuleta kiharusi.
kuongezeka uzito; kama nilivyosema hapo mwanzo kwamba chumvi
huzuia maji kutoka nje ya mwili, hii huongeza uzito wa mwili na kumfanya
mtu kujisikia amejaa tumbo muda mwingi, kumbuka lita moja ya maji
sawasawa na kilo moja ya uzito.
kupungua kwa uwezo wa mishipa ya fahamu; katika watu wenye umri
mkubwa chumvi inazidi kupunguza uwezo wao wa kufanya shughuli mbalimbali
na kujikuta wakitetemeka na kushindwa kubeba hata kikombe kimoja cha
chai.
magonjwa ya mifupa; mwili wa binadamu unapoteza kiwango cha
calcium mwilini pale mtu anapozidi kutumia chumvi zaidi, hii huweza
kusababisha mifupa kua milaini na kuvunjika kirahisi pale inapoangukua
kidogo tu.
mwili kushindwa kutoa mabaki mwilini; chumvi nyingi mwilini
huingilia mfumo wa mwili kuondoa mabaki ya uchafu mwilini, moja ya
mabaki yanayobaki ndani ya mwili ni uric acid ambayo inaweza
kusababishwa ugonjwa wa maumivu makali ya jointi kitaalamu kama gauti.
suluhisho ni nini? punguza sana kiasi cha chumvi kwenye mla wako
na baada ya muda utazoea, kwa wagonjwa wa presha ambao wanatakiwa wale
chumvi kidogo zaidi kuna chumvi maalumu kwa watu hao ambazo zinapatikana
mijini, chumvi hizi zina kiwango kidogo sana cha sodium hivyo presha
zao huweza kushuka
0 comments:
Post a Comment