Pages

Subscribe:

Sunday, April 2, 2017

STORY: NILIACHA USISTER NIKAWA MCHAWI 11

Image result for ROMAN CATHOLIC SISTER
“Mama,” niliita. “Nini?” “Si wewe umesababisha.” “Ni moja ya majukumu mwanangu, sasa twende nyumbani maana hata ushetani kwa wale uwatoke.” SASA ENDELEA… Hapa naomba nisema jambo moja kwamba, sehemu inapotawaliwa na balaa la damu, yaani hali ya kutaka damu imwagike mara nyingi huwa ni nguvu ya ziada inafukuta mahali hapo. Kwa kawaida nguvu hiyo hutoweka kwa uhalisia wa damu tu. Ndiyo maana baada ya yule mteja kuchomwa kisu na kuanguka, hata yule aliyemchoma mwenzake kwa kisu alikimbia. 

Unaweza kukuta watu wanazozana, wakiamuliwa hawasikii, hapo ujue pana mjumbe wa damu, lengo ni imwagike ili mambo mengine yaendelee. Utakuta watu wanatishana, wanawekeana viapo vya...
kukufuru na kutoleana maneno ya ajabu lakini wakishikana na kumwaga damu mambo yanasimama, ukimya unatawala na majuto huanza kujitokeza hapo. “Kwa nini nilimchoma kisu. 

Kwa nini sikuacha tu nikaondoka. Kwa nini nisitumie msemo wa kunguru mwoga hukimbiza bawa lake.” Hayo ni maneno baada ya tukio kutendeka. Lakini ukweli ni kwamba, roho wa damu anakuwa ameshapata alichotaka na kuondoka. Lakini nyuma au kando ya roho hiyo wachawi husimamia zoezi lote. Tulipofika tu nyumbani, swali langu la kwanza kwa mama lilikuwa hili: “Hivi mama, ni kwa nini kule kwa masista tulifeli?” Mama aliinua macho kuniangalia kwa kunitumbulia kisha akaonesha uso wa masikitiko makubwa sana, akasema: “Mwanangu, we acha tu. 

Mambo ni makubwa pale, tena tumshukuru Mungu kwani tungechelewa tungenaswa, tusingetoka hata kidogo mpaka asubuhi.” “Sawa mama, lakini hujanijibu swali langu.” “Lipi?” “Kwa nini tulikwama?” “Pana nguvu pale.” “Nguvu ya nani?” “Nguvu ya Mungu.” “Ilitokana na wale kuomba?” “Yule wa mwisho aliposema asante Yesu pale ndiyo palikuwa na tatizo kubwa sana. 

Mahali pa vile hatuwezi kupaingia sisi wachawi. Tunaweza kote lakini si mahali penye nguvu ya Mungu.” Mama akaendelea kunisimulia kwamba, wachawi wanaweza kuingia mahali popote pale isipokuwa kwenye eneo ambalo nguvu ya Mungu ni kubwa kama kwenye nyumba za kuabudia zenye upako. 

Upako ni utiisho wa Mungu. “Lakini mama jambo jingine ni kwa nini wachawi wanashindwa kuchukua pesa benki?” “Mwanangu bwana, una maswali sana leo. Hujui kwamba pesa nazo zinalindwa?” “Si na askari?” “Si askari. Wachawi wanashindwa kuchukua pesa popote pale. Watu wenye uwezo wa kuchukua pesa mahali ni waganga wa kienyaji. Ukimsikia mtu analalamika kwamba pesa zake zimechukuliwa ujue ni waganga wa kienyeji ndiyo wamezivuta lakini si wachawi.” “Kwa nini?” “Iko hivyo mwanangu.” “Kwa nini iwe iko hivyo mama?” “Unajua fedha zina tabia ya kujilinda.” 

“Kwa hiyo waganga wa kienyeji wao wana uwezo zaidi ya sisi wachawi?” “Ndiyo. Ukitaka kuamini ndiyo maana utakuta mtu akirogwa anakimbilia kwa mganga wa kienyeji. Mtu anaweza kurogwa akaponea huko. Hata mganga anaweza kumkamata mchawi.” “Sasa mama kwa nini tusiwe waganga wa kienyeji badala ya kuwa wachawi?” “Wachawi wana uwezo wa kimaarifa zaidi kama vile kutoonekana, kupaa angani lakini waganga hawawezi, ukimwona mganga anaweza kupaa angani basi naye ni mganga mchawi.” 

Ndani ya nyumba, watu waliokuwa si wachawi walikuwa wamelala fofofo huku wengine wakisikika wanakoroma. Tulilala. Bibi pia tulimkuta ameshalala kwa hiyo na sisi hatukumwamsha mtu. *** Asubuhi kulikucha, watu wote walikuwa wameamka, ndugu mmoja wa kiume akatuita wanawake na kuweka kikao nje. Alisema shughuli ya kulala nyumbani kama tanga ilikuwa inakoma siku hiyo, watu walitakiwa kurudi makwao na kubaki wahusika wakuu. 

Nilimwona mama akifurahia chinichini lakini sikujua alikuwa akifurahia nini kwani kwa wengine wanapofikiwa watu wakiondoka husikia majonzi zaidi. *** Baada ya watu kuondoka, nyumbani tulibaki watu wachache sana, mimi, mama, bibi, wadogo zangu na shangazi. Ilikuwa saa saba mchana wakati napika, ghafla nilimwona mama akiingia ndani kutoka nje kwa mwendo wa kasi kisha baada ya dakika kama kumi akatoka akiwa uchi wa mnyama. “Ha! Mama,” nilihamaki chini kwa chini wengine wasisikie. Hapo sikujua alipo bibi. 

Mama alitoka vile hadi nje kabisa ambako shughuli za watu zilikuwa zikiendelea kama kawaida jambo ambalo lilinitisha huenda akaonekana na kuumbuka. Kwa jinsi alivyokuwa nilisahau kabisa kwamba ni mchawi kwa hiyo atakuwa haonekani. Imani ya kwanza kwamba haonekani ilikuwa kwa wadogo zangu waliokuwa wamekaa nje, kwani mama alipita pale na kama wangemwona lazima wangepiga kelele. 

Ilibidi nisimame na kwenda mbio hadi nje. Nilimwona mama anacheza dukani, ng’ambo ya barabara huku akifanya staili nyingi za vituko vya hapa pale. Kila mteja aliyekwenda dukani pale, mama alicheza kumzunguka kona yote lakini bila mteja mwenyewe kujijua.Nilihisi mambo mabaya sana kama hali yenyewe ni vile. Hata pale mteja alipokuwa akitoka kwenye duka hilo, bado mama alimchezea mpaka kukanyaga barabara na kurudi tena dukani.

0 comments:

Post a Comment