Ugonjwa wa kuvuja kwa nyimbo ambazo
hazijakamilika au muda wake wa kutoka umekuwa ukizidi kukua siku hadi
siku na kupelekea wasanii wengine kuwa katika wakati mgumu wa ku-release
nyimbo zao tofauti na mipango yao.
Kwa mara kadhaa tumekuwa tukisikia nyimbo
za Yamoto Band zikisambaa mitandaoni kabla yakufika kwenye Platform ya
Radio. Yaani unashangaa nyimbo inakiki tu mitandaoni lakini...
hujawahi
kusikia wao waki-promote kuwa wameachia kazi mpaya. Mfano ni ile nyimbo
ya “Kidawa” ya Aslay. Kwa niaba ya Yamoto Band, Maromboso amepiga story
na sisi.
Akiongea wiki hii, Maromboso amesema “Inatokea
mtu kukuta nyimbo ila sasa sio kuvujisha, Unajua kuna kuvuja nyimbo na
kuvujisha. Kuvujisha ni kitendo ambacho kinafanyika makusudi, kuvuja
nyimbo nikitu ambacho kinatokea kwa bahati mbaya, ‘either’ kunamistake
zimetokea kwa maproducer au kuna mtu alichukua nyimbo akajitia yeye
ndiyo yeye akapeleka mjini”.
Aliongeza, “Kwa hiyo nikisema
kuvujisha nikitendo ambacho kimekusudiwa ila kuvuja nikitu ambacho kwa
bahati mbaya kwa hiyo nyimbo zetu sisi huwa zinavuja, either kwa sasabu
ya production tunayoifanyia kzi inakuwa haina ulinzi mzuri wa nyimbo.
Ila mimi ninavyojua tukifanya kitu sisi, tukirekodi kila mtu anakuwa na
shauku ya kutaka kusikiliza nini tumefanya, kuchukua labda na kwenda
kusikiliza nyumbani kwa hiyo ilo nalo linachangia mwisho wasiku goma
linafika kwenye social network”.
0 comments:
Post a Comment