Wednesday, April 5, 2017
WHATSAPP KUANZISHA HUDUMA YA KIFEDHA
Huduma ya kutuma ujumbe kubwa zaidi duniani, WhatsApp, hivi karibuni itawaruhusu makumi kwa mamilioni ya watumiaji wake kutuma kitu muhimu zaidi ya picha ama video – fedha. WhatsApp inailenga zaidi India, soko lake kubwa zaidi kwa uwezekano wa kuingia katika malipo ya mtandaoni. App hiyo inayomilikiwa na Facebook, inaajiri mkurugenzi wa kuongoza jitihada hizo za malipo ya dijitali katika nchi hiyo ya Kusini mwa Asia.
Huduma hiyo itashirikiana na mabenki katika kusaidia miamala ya kidijitali kwa kutumia WhatsApp. India ina watumiaji wa WhatsApp milioni 200 kila mwezi ambayo ni...
moja ya tano ya watumiaji wake wote hivyo si jambo la kushangaza kuona imelengwa yenyewe kwanza.
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment