Msanii wa kiwango cha kimataifa, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ hivi
karibuni alijikuta akilikoroga kwa Waislamu baada ya kutupia mtandaoni
vito mbalimbali vya madini ya dhahabu na almasi vilivyomo mwilini mwake
kisha kujigamba kuwa ametumia kiasi cha shilingi 158,000,000.
Baada ya majigambo hayo, baadhi ya watu walianza kutupia comments zao,
wengi wakimpongeza kwa mafanikio aliyopata lakini wengine wakahoji
sababu za kutumia pesa nyingi kwenye vitu hivyo wakati... kuna watu wenye
shida wanaohitaji msaada wake.
“Ya nini utumie pesa nyingi hivyo kwenye vitu hivyo kaka, wapo watu
wana shida, wanalala na njaa, wewe unatumia pesa zote hizo kwenye hiyo
anasa, angalia jinsi ya kuwasaidia wenye uhitaji…” aliandika shabiki
mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Twizzda1.
Baada ya shabiki huyo kuandika hivyo, ndipo zikaanza meseji ambazo
zilikuwa zikimtaka msaniii huyo kuweka utaratibu mzuri wa kusaidia jamii
ikiwa ni pamoja na kutoa sadaka.
Kufuatia wengi kuonesha kumshutumu kutotumia vizuri pesa zake kwa
kuwasaidia watu wenye shida, akiwemo mtu mmoja aliyejitambulisha kwa
jina la kimtandao la @the_holyday, uzalendo ulimshinda Diamond na kuamua
kufunguka mambo ambayo yalionesha kuwakoroga Waislamu.
Diamond aliandika hivi: @the_hoyday nimejenga nyumba 5 mwaka jana
Iringa, misikiti miwili, mmoja Moro na pia mwingine Mtwara na madrasa
Tegeta na nyumba ya imamu, sadaka mbalimbali, sasa unataka nitoe hela
zote sadaka nami nisifurahishe nafsi yangu, hembu niombe radhi kwa hilo.
Baada ya kuandika maneno hayo, ndipo wadau mbalimbali, baadhi wakiwa ni
waumini wa dini ya Kiislamu walipokorogwa na kuanza kueleza kuwa,
anachokifanya Diamond siyo taratibu za dini yao.
“Miongoni mwa taratibu za Kiislamu katika kutoa sadaka, hutakiwi
kuitangaza, inatakiwa ibaki siri yako na Mungu wako, unapotangaza kwamba
umefanya hivi na vile unatarajia nini, hii siyo sawa Diamond…”
aliandika mmoja wa wachangiaji.
Mwingine akaandika:
“Hapa ulipofikia siyo, unaanzaje kujitangaza hivyo, ni kweli umefanya
mambo makubwa sana ambayo thawabu zake si ndogo, lakini unakwenda
kinyume na taratibu za dini, ukishatangaza hivyo na watu wakajua
umefanya yote hayo, lazima watakusifia lakini ujue kwa Mungu huna chako…
huna chako kwa kuwa, si tayari umeshasifiwa duniani.”
Hata hivyo, mmoja aliyeonesha kuwa na busara ali-comment hivi:
Diamond, uliyofanya ni mambo makubwa sana, malipo yake si madogo na
ndivyo inavyoshauriwa kwa wale waliojaaliwa kuwa nacho kutoa zaka na
sadaka pale inapobidi, ulichokosea ni kujitamba mtandaoni, unaweza
kutubu kwa hilo. Baada ya Waislamu wengi kutokwa na povu kufuatia
kitendo cha Diamond kujitangaza mambo aliyoifanyia dini yake na hili la
kuvaa vito vya bei mbaya,
Ijumaa lilimtafuta Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar, Alhad Musa Salum ambaye alisema:
“Kwanza kwa mtoto wa kiume kuvaa vitu hivyo ni haramu halafu hili la
kujitangaza mambo aliyofanya itategemea amefanya hivyo kwa nia gani,
kama nia ilikuwa kuwafanya watu wajue tu kafanya hayo ndani ya Uislamu,
hiyo ni ria na ria siyo kitu kizuri hata kidogo. “Lakini pia anaweza
kuwa amefanya hivyo ili kuwahamasisha wengine wafanye, hilo si tatizo.
Kwa hiyo hapo itategemea na nia yake.”
0 comments:
Post a Comment