Sunday, April 2, 2017
MIMI MARS: HUWA NAJISKIA VIBAYA NINAPOAMBIWA NAFANANA UIMBAJI NA VANESSA MDEE
Kwa wanaume wanaomtamani Marianne Mdee aka Mimi Mars, waombe wasikutane na kigingi cha dada yake, Vanessa aka Vee Money.
Mimi amekiri kuwa Vee ni dada mkali ambaye huhakikisha mafisi hawapati muda rahisi wa kumchezea mdogo wake. Akiongea kwenye kipindi cha FNL cha EATV, Mimi alisema hata hivyo wapo wanaume ambao hujaribu kupitia...
kwa Vee ili kujitafutia nafasi za kukaa kwa mdogo wake huyo mrembo.
Katika hatua nyingine, Mimi alidai kuwa huwa akijisikia vibaya kiasi kuambiwa kuwa ana sauti ya uimbaji kama ya dada yake. Amesema kimsingi yeye na Vee wana utofauti wao katika kutengeneza nyimbo zao japo amekiri kuwa kuna ufanano mdogo kwenye wimbo wake Shuga. Amesema kuwa katika nyimbo zake zijazo, tofauti itaonekana.
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment