Thamani ya Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika
timu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta imepanda katika soko la
wachezaji duniani. Thamani
yake kwa imefikia kiwango cha Euro milioni 3 sawa na shilingi bilioni
7.1 za kitanzania kwa mujibu wa mtandao unaohusika na biashara za
wachezaji duniani.
Hatua hiyo imekuja baada ya Samatta
kutimiza idadi ya kiwango cha magoli iliyokuwa ikihitajika ambapo
ameweza kufunga mabao saba katika mechi sita za hivi karibuni akiwa
katika timu yake ya Genk pamoja na...
mawili aliyoyapachika Botswana mchezo
uliochezwa na Taifa Stars.
Mabadiliko hayo yamefanyika mwishoni mwa
mwezi Machi ambapo mshambuliaji huyo alionekana kung'ara katika ushindi
wa bao 4-1 iliyopata klabu yake dhidi ya Lokeren na yeye akitupia bao
mojawapo.
Ikumbukwe Samatta alinunuliwa na TP
Mazembe akitokea Simba kwa thamani ya Euro 70,000 na kisha kuuzwa Genk
kwa Euro 500,000 na sasa timu yoyote ikimuhitaji italazimika kutoa Euro
milioni 3.
0 comments:
Post a Comment