Eric Shigongo, mfanyabiashara maarufu na mmiliki wa kampuni ya Global Publishers Baada
ya kufunguka mengi kuhusu Diamond na uongozi wake na mwishowe kuambulia
matusi ya kila namna kutoka kwa mashabiki wa staa huyo, hatimae Eric
Shigongo sasa amvaa Alikiba na uongozi wake.
Shigongo kaamua kumshauri Alikiba
kuhusiana na muziki wake na namna ambavyo anatakiwa kuishi kwa mipango
ili hata siku asipokuwepo kwenye ramani ya muziki awe na...
maisha yenye
tija kulingana na kazi alizofanya nyuma.
Kwanza kabisa nianze kwa kukiri kuwa
sikuwahi kukutana na Ali kiba ana kwa ana mpaka miezi miwili iliyopita
nikiwa katika Hotel ya Double Tree, iliyopo Masaki, Jijini Dar Es
salaam.Nilikwenda pale kwa ajili ya chakula cha mchana na mke wangu.
Muda mfupi tu baada ya sisi kuingia walifika Ali Kiba na Meneja wake
Christine Mosha (Seven) wakaja moja kwa moja kwenye kona tuliyokaa na
kutusalimia.
Kitu cha kwanza nilichojifunza na
kukipenda kwa Ali kiba ni unyenyekevu, kijana huyu ni mnyenyekevu
mnoooo! Kitu hiki peke yake ukiachana na muziki wake kilinifanya
nimpende Kiba. Walipoondoka mimi na mke wangu wote tulikiri KIBA NI
MNYEYEKEVU NA NDIYO SABABU AMEFANIKIWA SANA KATIKA MUZIKI.
Tunapoongelea mafanikio ya Kiba kamwe
hatuwezi kuacha kumpongeza meneja wake, hongera Seven. Msichana huyu
mdogo ni humble, smart, intelligent and clever! Bila Shaka ndiyo siri
kubwa ya mafanikio ya Kiba katika muziki.
Wiki chache baadae Ali kiba alishinda
Tuzo ya MTV huko Africa Kusini na kuliletea taifa letu sifa kubwa sana!
Sikuwepo uwanja wa ndege wakati wa mapokezi yake lakini Globaltv Online,
walitengeneza ‘Documentary’ nzuri sana iliyoonyesha jinsi kijana huyo
alipokelewa kifalme na mamia ya vijana, kuliko ambavyo hata timu yetu ya
taifa hupokelewa, BRAVO KIBA.
Makundi ya vijana walikuwepo uwanja wa
ndege kuonyesha mapenzi yako kwa Kiba, vijana wa kawaida, wanaishi
maisha ya kawaida, wafanyabiashara ndogondogo, wanafunzi n.k. Hapakuwa
na mfanyakazi wa CRDB, BOT ana Standard Chartered mahali pale! Sikuona
aliyefunga tai na shati jeupe mahali pale.
Gari ya Kiba ilisukumwa, vijana wale
walijichangisha elfu moja moja mpaka kutimiza pesa ya mafuta ya gari la
Kiba! Hakika hii ni ishara ya upendo mkubwa kwa Kiba.
Leo nitamshauri Ali Kiba! Si kila mtu
atataka ushauri, si kila mtu anapenda kushauriwa. Hata ukimwambia mlevi
acha pombe, atakuchukia, hata ukimwambia mvuta sigara aachane na sigara
kwa kuwa inaua, atakuchukia, kuchukiwa ni sehemu ya maisha yetu,
haikuanza jana, juzi, na haitoishia kesho, bado itaendelea kuwa hivyo
vizazi mpaka vizazi. Baada ya kumshauri Diamond leo nataka nimshauri Ali
Kiba. Sijui kama atafurahi au atachukia, ninafanya hivi kwa kuwa sitaki
waache muziki hapo baadaye huku wakiwa hawana kitu. Sitaki baadaye mtu
aseme kwamba kuna watu waliwatumia, wakaingiza pesa halafu wamewakimbia.
Baada ya kusema hayo hebu niongee
kilichonisukuma kuandika hiki ninachokiandika, ni ushauri, Kiba na
meneja wake wanaweza kuuchukua ama kuuacha! Si lazima, kama mhamasishaji
wa watu kujiondoa katika umasikini ninaona kama ninao wajibu wa
kumshauri Kiba nikiwa kama kaka, anko au Mtanzania mwenzake, naamini kwa
hekima walizonazo Ali Kiba na meneja wake bila shaka watapata la
kuchukua, yasiyofaa wataniachia mwenyewe.
Nampenda Kiba sana tu na ninajivuna sana
kuwa Mtanzania mwenzake na ningependa kuona anafanikiwa zaidi katika
kazi yake. Kama siwezi kufurahi mafanikio ya Watanzania wenzangu basi
hakuna haja ya mimi kuzunguka huku na kule ndani na nje ya nchi yangu
kuhubiri injili ya mafanikio, watu watoke kwenye umasikini unaolitesa
taifa langu. Haikutokea tu Ali kiba akawa anapendwa vile, la hasha, ni
matokeo ya vitendo fulani ambavyo amekuwa akivifanya maishani mwake
mpaka Akawavuta watu kumpenda! Mambo hayo hayo akiyaacha hata followers
wa Instagram wanaomfanya ajisikie anapendwa leo wataondoka!
Ali kiba, meneja wake na Watanzania
wenzangu lazima mnisikilize hapa; MAFANIKIO MAISHANI HUJA NA KITU NYUMA
YAKE, mara nyingi kitu hicho huwa kuwapuuza na kuwadharau waliokufikisha
ulipo. Kuwatenga bila kufahamu hao ndiyo wanunuzi wa kazi zako ama
wasikilizaji wa muziki wako na wakikuachia tu utatumbukia shimoni na huo
ndiyo utakuwa mwisho wako.
Ali kiba anapaswa kufahamu kwamba hawezi
kuwa Champion for life, hata akiwa bora kiasi gani lazima siku moja
atakuja mtu bora zaidi yake. Kabla ya Chris Brown alikuwepo Usher
Raymond, kabla ya Rihanna alikuwepo Beyoncé, kabla ya Floyd Maywether
alikuwepo Mike Tyson, kila zama na bingwa wake. Leo ni Kiba kesho
atakuwa mwingine, swali la kujiuliza ni kwamba: SIKU ALI KIBA
ATAKAPOKUWA NJE NANI ATABAKI NAYE? Sasa hivi gari lake linasukumwa na
anazungukwa na watu kila anakokwenda, lakini ipo siku atakuwa si maarufu
tena kama ilivyotokea kwa Mr Nice, Inspector Haroun na wengine wengi!
Atafanya Nini kiba siku atakapokuwa
anakaa kwenye meza hotelini viti vingine vyote havina watu? Hakuna
mpambe? Au Meneja? Haya mambo yatatokea ndugu zangu….
0 comments:
Post a Comment