Mkongwe wa bongo fleva Juma Kassim Nature ‘Sir Nature’ amekanusha vikali kulipwa na msanii Harmorapa
katika wimbo wa ‘Kiboko ya mabishoo’ na kudai kwamba kijana huyo hana
pesa za kumlipa na kusisitiza yeye alifanya kwa upendo tu.
Nature amesema kwamba alikubali kushiriki
katika wimbo huo kwa sababu anaamini msanii huyo chipukizi ana uwezo
mkubwa ikiwa ni pamoja na kuamini...
atafika mbali.
“Nikisema nimemlipisha Harmorapa
pesa kwa ajili ya kolabo nitakuwa nakosea, mimi ni mtu mzima nilikubali
kufanya wimbo na msanii yule kwa sababu ni mkali na anajua muziki pia na
imani atafika mbali, hawezi kunilipa mimi, ana hela gani”. Alisema Juma Nature ndani ya EATV.
Katika hatua nyingine Nature kutoka TMK amesema yeye ameshakuwa mkongwe hivyo vijana kama kina Harmorapa wanapotokea kwenye ‘game’ inamlazimu kutoa sapoti ili hata watakapoondoka kuwe na watu wa kuendeleza muziki.
Aidha Nature amekanusha kusikia taarifa
ambazo Harmorapa alidai kuwa amemlipa Nature kwa kolabo na kuongeza hizo
taarifa kwa upande wake hazimkufikia rasmi.
Hata hivyo Harmorapa aliwahi kunukuliwa
akisema siyo busara kwa wasanii wakongwe kuwalipisha pesa wasanii
wachanga kwa kuwa ndiyo kwanza wanaanza kutafuta pa kutokea na kuweka
wazi kuwa kwa upande wake alilazimika kumnunulia nguo Nature za kufanyia
video ya ‘Kiboko ya Mabishoo’.
0 comments:
Post a Comment