Msanii Roma Mkatoliki amesema hali ya utandawazi imeharibu nchi ya
Tanzania katika utendaji kazi maofisini mpaka shuleni kutokana na watu
kutekwa na mitandao ya kijamii kwa kutotaka kupitwa na vitu
vinavyoendelea kutokea.
Akizungumza
katika kipindi cha eNewz kinachorushwa na EATV rapa huyo anayetamba na
ngom ya 'Usimsahau Mchizi' ametoa kauli hiyo kufuati hali ya nchi
kukumbwa na...
matukio makubwa ya kisiasa kila kukicha na kupelekea kila
mwananchi kutamani kuona au kusikia mwenyewe.
“Hali ilipofikia sasa hivi
ni heri mtu akose figo kuliko bando nikimaanisha kwamba nguvu ya
mitandao kijamii imekuwa kubwa sana kiasi kwamba ukienda mashuleni,
maofisini utakuta watu saa 12 asubuhi wakiripoti maeneo yao, mchongo wa
kwanza utakuta mtu anakwambia ebwana umeona fulani instagramu ameandika
nini, kitu kama hicho kuanzia mwaka 2012 kushuka chini sijawahi kukiona”. Alisema Roma
Aidha msanii huyo amejitolea mfano kwa
kusema imefikia hatua endapo wanapokutana na washkaji zake basi ndani ya
dakika 40 wote wanajikuta wamepiga ukimya (ganzi) kila mtu huwa yupo
‘busy’ na simu yake kuangalia ‘ubuyu’ katika mitandao ya kijamii.
Kwa upande mwingine Roma amefafanua ile
kauli yake aliitoa kuwa ‘tunajenga Tanzania ya viwanda au Tanzania ya
ubuyu’ na kusema laiti kama watanzania wote wangekuwa wapo pamoja katika
kutazama huko basi lengo hilo la kubadirisha nchi ingekuwa nyepesi
lakini sasa hivi imekuwa tatizo kubwa kutokana watanzania wengi kuwa
hawajapewa nafasi ya kutoa mawazo yao katika kuiboresha na kuijenga
dhana hiyo katika nafasi inayostahili.
0 comments:
Post a Comment