1. Magonjwa ya "Urinary tract infection" au UTI hayataisha kwako. Hii
hasa ni kwa wanawake wanavaa nguo nyingi kwa wakati mmoja na kwa muda
mrefu zaidi ya saa kumi. Unavaa chupi, lakini tight, suruali ya jeans,
nk halafu unashinda na hizo nguo kuanzia asubuhi unapoenda kazini hadi
saa mbili usiku unaporudi home.
Hiyo ni hatari sana. Mwanamke anayefanya
kazi zinazompasa kuwepo kazini zaidi ya masaa 8 anashauriwa asiwe anavaa
chupi kabisa. Chupi ivaliwe nyakati za hedhi tu. Kama hauko kwenye siku zako vaa...
suruali tu bila chupi. Au vaa underskirt
pekee yake kwa ndani na ndoo uvae nguo yako ya kawaida.
Hii itakuepusha na kuugua UTI. Ukiacha sababu za ngono UTI husababishwa
na bacteria wanaopendelea mahali penye unyevu na joto. Kwa hiyo mwanamke
akivaa nguo nyingi bacteria hao hujipatia joto la kutosha kuzaana.
Mwanamke ni vyema ukaepuka kuvaa nguo za kubana mwili sana ili kuepukana
na uwezekano wa kupafanya ukeni pawe na joto sana na ikitokea bacteria
mmoja tu akaingia humo atazaa haraka sana na kujikuta UTI inakuwa rafiki
yako. Vaa sketi bila chupi au kama kuvaa suruali ni lazima hakikisha
unavaa suruali peke yake. Jizoeze tu utazoea. Na ukizoea kuvaa nguo bila
chupi utainjoi sana.
2. Magonjwa ya kuvu au fungus hayatakoma kwako. Bado niko kwa wanawake,
kama nilivyoeleza mwanzo hapo magonjwa ya fungus yanasababishwa pia na
kuvaa chupi kwa muda mrefu. Chupi inayovaliwa kwa zaidi ya saa 8 lazima
italeta ukungu au uvundo sehemu nyeti. Huo uvundo waweza kuleta fungus
ukeni. Fungus za ukeni hazina tofauti na zile za miguuni kwa wanaume
wanaovaa viatu kwa muda mrefu bila usafi miguuni wa kutosha. Chupi
inakuwa kama socks za wanaume. Mwanamke avaae chupi muda mrefu bila
kuruhusu upepo upite ndani ni watapata fungus ukeni sawa na mwanaume
anayevaa socksi zisizofaa kiafya.
Chupi au socks zinazofaa ni zile za pamba au cotton. Of course sababu za
kupata ugonjwa wa fungus kwa mwanamke siyo tu kuvaa chupi inayobanaaaa
kwa muda mrefu ni pamoja na kutawadha kwa kutumia maji. Wanawake wengi
hawajui kutawadha kwa kutumia maji.
Friday, March 31, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment