Kukubali kile ambacho
mwingine anacho ni moja kati ya ishara na namna fulani ambayo inaonyesha
kuwa mwanadamu amekomaa kifikra na kiakili kuwa pamoja kuwa anajikubali
juu ya uwezo wake lakini anaweza kumpa mwingine heshima yake
inapostahiki kufanya hivyo.
Ipo wazi Msanii kumsifia msanii mwenzake hata kama hawajawahi fanya pamoja collabo ni kazi sana hasa kwa wasanii wakike. Msanii wa muziki kutoka THT, Nandy ambaye anafanya vizuri na single ya ‘One Day‘amesema...
anavutiwa na jitihada za msanii mwenzake, Vanessa Mdee, kwa namna anavyoiwakilisha vyema Tanzania kimataifa.
Akiongea na Gazeti la Dimba wiki hii,
Nandy amesema, Vanessa anajua anachokifanya kimataifa kwani licha ya
kupiga mkwanja wa kutosha kupitia shoo zake lakini amekuwa balozi bora
wa tasnia ya muziki wa kizazi kipya.
“Unajua mtu anapofanya vizuri ni
lazima apongezwe, ukweli mimi navutiwa sana na kazi za Vanessa, amekua
akifanya kazi kwa kujiamini sana na hakati tamaa, amekuwa akituwakilisha
vyema kimataifa hasa sisi wasanii wa kike, kwangu huyu ni role model
wangu,” alisema Nandy.
Alisema wasanii wa kike kwa sasa wamekuwa
na ushindani kwenye gemu hali inayoongeza hamasa zaidi kwa wengine
kutamani kuingia kwenye muziki.
0 comments:
Post a Comment