Imebainika sababu ya kundi la Yamoto Band kuamua kila msani kutoa
wimbo wake ni baada ya msanii Aslay kutoa wimbo ‘Kida’ bila ruhusa ya
uongozi wa kundi hilo na bila kushauriana na wenzake.
Akizungumza na EA Radio katika kipindi cha Planet Bongo, msanii Beka
amesema baada ya Aslay kuchukua hatua hiyo nao walishawishika kufanya
hivyo ndipo...
walipoomba ruhusa hiyo kwa uongozi na kukubaliwa kufanya
hivyo.
“Kile kitu kilifanya tujiulize kwa nini huyu katoa ngoma sisi wengine
tukikaa kimya tutaonekana kama hatuna uwezo wa kufanya kitu, ebu nasisi
tufanye lakini hatukutaka kufanya kama alivyofanya yeye, basi tukaomba
uongozi wetu na kukubaliana, Mkubwa akasema mnakuwa mnajiongeza na
kujikuza kwenye muziki,” amesema Beka.
Beka ameongeza kuwa zamani watu walikuwa wanawaomba kila mmoja atoe
wimbo wake lakini kwa wakati huo walishindwa kujibu maombi yao.
Friday, June 2, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment