Pages

Subscribe:

Friday, February 16, 2018

DAKTARI WA SIMBA ATOA TAARIFA JUU YA HALI YA JOHN BOCCO



Daktari wa klabu ya Simba SC, Yasin Gembe amesema kuwa hali ya nahodha wa timu hiyo, John Bocco inazidi kuimarika ukilinganisha na ilivyokuwa hapo jana kufuatia kupata majeraha wakati wa mchezo wao dhidi ya Mwadui FC.

Katika maelezo yake na mtandao wa klabu hiyo, Gembe amesema kuwa mapema asubuhi yaleo wamekwenda hospitali kupata...
matibabu ya awali

“Akiongea na mtandao wa klabu hiyo, Daktari wa kikosi cha Simba, Yasin Gembe ametoa maelezo ya kwanza kuhusiana na hali ya nahodha John Bocco. ‘Bocco anaendelea vizuri tofauti na hali ilivyokuwa hapo jana, leo asubuhi tulikwenda tena hospitalini kupata matibabu ya mwanzo. Hali yake inaendelea vizuri na tutakapofika Dar es Salaam tutafanya uchunguzi wa kidaktari na matibabu zaidi’ alisema Dkt. Yassin Gembe.

Bocco aliumia jana kwenye mchezo dhidi ya Mwadui FC baada ya kuchezewa rafu na Rovacatus Richard ambapo ilimlazimu kutoka na nafasi yake kuchukuliwa na Laudit Mavugo hata hivyo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2.

0 comments:

Post a Comment