Muigiza, mchekeshaji na mtangazaji wa Radio, Idris Sultan ametangaza ujio wa tour yake ya vichekesho iitayo ‘NOT FUNNY TOUR 2018’ itakayoanza mwezi wa nne mwaka huu.
Kupitia mtandao wa kijamii wa instagram, Idris ameweka bayana mikoa kama Dar Es Salaam, Arusha, Mwanza, Dodoma na...
Zanzibar kuwa ndiyo itakayoweza kufanikiwa kuona tour hiyo ya vichekesho.
“Mda wetu wa kuvunja records in selling out tickets umefika .. Mwaka mzima nilitulia kufanya stand up comedy tangu we sold out 800 Mwanza. Sasa chonde chonde hii show itakua motoooo sanaaa you don’t wanna miss. APRIL One Mic one Man na sina mpango wa kuwaacha wazima.
Ntatangaza tarehe soon, let’s make Tanzania laugh. I promise you hii inavunja record thanks to you. Nitakua natangaza uwanja nyie kazi yenu moja tu hakikisheni panajaaaaaaaaa. NOT FUNNY TOUR 2018, hatujaja kucheza LET’S BREAK RECORDS !!! #NotFunny2018,” ameadnika Idris.
Kwa sasa msanii huyo pia anajiandaa kuingia kambi kwa ajili ya filamu ya ‘The Blue Maurtius’



Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment