Pages

Subscribe:

Sunday, February 4, 2018

KUNDI LA VIJANA WAVAMIA HOSTEL NA KUBAKA NAWAFUNZI

Polisi katika eneo la Embu Magharibi nchini Kenya, wameanzisha uchunguzi wa tukio la kubakwa kwa wanafunzi watano wa vyuo, baada ya kuvamiwa na kundi la vijana takriban 10 na kuwaibia mali zao na kisha kuwabaka. 

Wanafunzi hao ambao wanaishi hostel huku wakiwa wa vyuo tofauti vya Chuka University, Chuo Kikuu cha Embu, Chuo cha mafunzo ya Madawa cha Kenya, walivamiwa na kundi la vijana wakiwa na mapanga usiku wa...
Februari 2 katika eneo la Bondenu huko Embu, na kuwapora vitu vyao kabla ya kuwachukua watano na kwenda kuwabaka.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mmoja wa wanafunzi hao ambaye jina lake halikuwekwa wazi, amesema kwamba watu hao walipoingia hostel usiku, walichukua simu, pesa, laptops, mitungi ya gesi na vitu vingine vya thamani, na kisha kuwafanyia kitendo hicho cha kikatili.

Hostel hiyo ambayo iko umbali wa mita 100 kutoka kituo cha polisi cha Embu Magharibi, waliingiwa na hamaki baada ya kuona simu zao hazipokelewi, na hata majirani hawausikia kelele zao.

Kamisha wa Kaunti ya Embu Esther Maina amesema tukio hilo limechelewa kupatiwa msaada wa kipolisi licha ya kuwa karibu, kutokana na polisi hao kuwa wamelala wakati wa kazi, na kwamba wanafunzi hao wamepekwa hospitali kwa matibabu.

0 comments:

Post a Comment