Imeripotiwa kuwa Liverpool baada ya kumsajili Naby Keita ambaye anacheza namba nane, wanahitaji kiungo mkabaji aina ya Victor Wanyama kwa ajili ya kuboresha kikosi chao, hivyo Wanyama anahusishwa kwa karibu kama...
chaguo namba moja.
Liverpool wanadaiwa kufuatilia kwa karibu maendeleo ya Victor Wanyama ambaye ndio amerudi kutoka majeruhi, Wanyama baada ya kupona amepata nafasi ya kuanza game za FA dhidi AFC Wimbledon na Newport County lakini amekuwa akitumika kama mchezaji wa akiba kwa game nane za Spurs toka apone jeraha la goti.
Wanyama alicheza kwa dakika 12 akitokea benchi game dhidi ya Liverpool na kuifanya game kumalizika kwa sare ya magoli 2-2, hivyo kuhusishwa kuondoka kwa Emre Can kwenda Juventus mwisho wa msimu kunazidisha tetesi kuwa maendeleo ya Wanyama yakizidi kuwa mazuri Liverpool watahitaji huduma yake lakini Man United na Chelsea wanahusishwa nae pia.



Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment