Pages

Subscribe:

Monday, February 5, 2018

RIHANNA ATUA NCHINI SENEGAL KWA NIABA YA CLARA LIONEL



Muimbaji wa muziki Rihanna ameungana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kuboresha elimu katika mataifa yanayoendelea.

Wawili hao wamekutana nchini Senegal wiki hii katika mkutano wa Global Partnership for Education, mkusanyiko ambao ulihusisha rais wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim na viongozi wa...
mataifa kadhaa ya Kiafrika.

kulingana na ABC News, Rihanna alienda nchini huko  kwa niaba ya msingi wa Clara Lionel  ambayo inafanya kazi katika mataifa maskini ya kutoa huduma za afya na programu za kielimu.

Mwimbaji huyo aliyezaliwa Barbados ni kama balozi wa kikundi hicho cha kimataifa.
“Kazi yetu haiwezi kuisha,” Rihanna aliwaambia wasikilizaji. “Na  hatuwezi kuacha kupigana hadi kila kijana na kila msichana aweze kupata elimu.”

Macron na Rihanna hapo awali walikutana huko jijini Paris  nchini Ufaransa  ambapo wawili hao  walijadili elimu na msingi wake wa kutoa huduma kwa kuendeleza elimu duniani kote.
Mkutano huo umefanyika ili kukusanya fedha kwa ajili ya elimu katika mataifa masikini. Wakati wa mkutano huo, Macron aliahidi kuwa Ufaransa inaweza kuchangia kiasi cha  dola milioni 248  na kuwaita viongozi wengine wa ulimwengu kutoa mchango pia.

“Kusaidia elimu sio chaguo ambalo  tunaweza kufanya au  kutofanya, ni lazima,” Macron alsema hivyo wakati wa mkutano huo”

0 comments:

Post a Comment