Wakizungumza kwa nyakati tofauti mastaa hao walifunguka kuwa, kwa kipindi hiki cha mvua ndiyo muda sahihi wa kusaka mtoto hivyo wanalifanyia kazi suala hilo kwa... nguvu zao zote.
“Tupo bize kidogo, tunasaka mtoto maana si unajua watu wanaangalia matunda ya ndoa kwa jicho la tatu hivyo sisi tunaangaika na hilo sasa hivi,” alisema Dogo Janja.
Kwa upande wa Uwoya alisema kuwa, yeye kama mwanamke anatakiwa kumzalia mumewe mtoto na hivyo kwa hivi sasa yeye na mumewe wapo katika harakati hizo kwa sababu Krish ameshakuwa mkubwa.
“Mke lazima amzalie mumewe na mimi na mume wangu sioni tunachosubiri kwa sasa maana Krish ni mkaka mkubwa na anahitaji mdogo wake,” alisema Uwoya.
0 comments:
Post a Comment