
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa rasmi wa Facebook wa kituo hicho cha Radio, MaDj hao maarufu mjini Detroit, DJs BiGG na Shay Shay Say wamesema kuwa...
wamefikia maamuzi hayo baada ya kuona kuwa maoni aliyotoa Kanye West kuwa watu weusi walichagua kuwa watuma yamefika mbali sana.
“Imetosha kwa sasa, hatutaki tena kusikia wala kucheza nyimbo za Kanye kwenye kipindi chetu, hatutamzungumzia tena Kanye West. Kwa hili tunasimama wima kwa pamoja na hatutacheza nyimbo zake, tumekataa kumpa platform kabisa.“imeeleza taarifa yao waliyoitoa MaDJ hao.
Rapa Kanye West mnamo Mei 01, 2018 akiwa kwenye mahojiano na mtandao wa TMZ alinukuliwa akisema kuwa “Watu weusi walichagua kuwa watumwa kwa miaka 400” .
Soma zaidi – Chris Brown amchana Kanye West kupitia mahojiano ya Will.i.amHata hivyo, Kanye West bado ameendelea kutetea maoni yake kupitia ukurasa wake wa Twitter akidai kuwa alimaanisha kwa kizazi cha sasa cha jamii ya watu weusi kuishi na mawazo hayo ya kutawaliwa miaka ya nyuma ni utumwa pia.
0 comments:
Post a Comment