Pages

Subscribe:

Wednesday, August 22, 2018

JESHI LA UGANDA LAOMBA RADHI KWA KUMPIGA MWANDISHI WA HABARI




Baada ya video ikiwaonesha Askari Polisi nchini Uganda wakimshushia kichapo Mwandishi wa Habari wa shirika la utangazaji la Reuters nchini humo, James Akena kusambaa mitandaoni. Hatimaye Jeshi hilo limeomba radhi kwa kitendo hicho.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini humo IGP Martin Okoth Ochola amesema kuwa...
Jeshi la polisi kazi yake ni kuhakikisha raia wake wanakuwa salama kwa kuwalinda na sio kuwanyanyasa kama video hiyo mtandaoni inavyoonesha.

“Nimepata mafunzo ya Uchunguzi na Upelelezi (CIP) kwa zaidi ya miaka 10, nimelitumikia pia jeshi la polisi kwa miaka 3o lakini sijawahi kumnyanyasa wala kumpiga raia. Nashangaa kwanini polisi wanamtesa raia? jukumu lao ni kumkamata tena bila hata ya kumpiga kwani hata wao wanajua kitendo hicho ni kosa kisheria na kinyume na maadili ya Upolisi,“amesema IGP Ochola.

IGP Ochola amesema kuwa amesikitishwa na kitendo hicho na amewaomba radhi wananchi kwa niaba ya jeshi la polisi na tayari ameeleza kuwa Polisi wawili wanashikiliwa tayari kwa kupelekwa mahakamani.

Akena alipigwa na kujeruhiwa vibaya na polisi wakati wa maandamano ya wananchi mjini Kampala wakipinga kitendo cha kukamatwa  Mbunge wa jimbo la Kyadondo, Bobi Wine ambaye pia ni mwanamuziki mkubwa nchini humo.

0 comments:

Post a Comment