Ilianza kama utani lakini siku zilivyosonga ndivyo uhusiano wao
ulivyowekwa wazi, hao ni watu wawili waliowahi kuwa maadui wakubwa miaka
kadhaa nyuma.
Hapo nawazungumzia staa wa filamu Shamsa Ford na msanii wa Bongo Fleva,
Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ambao kwa sasa wamezama kwenye mahaba
niue.
Awali, wahusika wote walitumia nguvu kubwa kukanusha juu ya uhusiano wao
lakini inatajwa kuwa mahaba yao ndiyo... gumzo kuliko ya wengine wote katika
Bongo Muvi na yanashika nafasi ya pili katika Bongo Fleva nyuma ya Diamond
na Zari kwa sasa.
Awali, uadui wao ulitokana na Nay kuwaponda wadada wa bongo movie na kudai wengi wao hawana lolote na kazi yao ni kujiuza,
Shamsa alikuwa mmoja wa waliopokea kwa hasira kali na kumbwatukia Nay
lakini ule usemi kuwa ‘wagombano ndiyo wapatanao’, ulikuwa unawahusu.
Walipoulizwa juu ya mahabati yao baada ya picha kuvunja
mitandaoni wakipeana ‘mabusu’ motomoto hivi karibuni, walisema wana
‘project’ maalum ya filamu.
Sasa inavyoonekana filamu yao imekuwa ya ukweli badala ya zile za kuigiz
0 comments:
Post a Comment