Abdu amedai kuwa wakati wa tukio hilo hakuwepo nyumbani na alipigiwa simu na kaka yake akimuomba msaada kwa kudai kuwa nyumba yake imevamiwa. Kutokana na simu hiyo, Abdu alirejea nyumbani haraka na bahati nzuri wakati akielekea nyumbani alikutana na gari la polisi alilolipa taarifa aliyopokea kutoka kwa kaka yake na kuongozana nao.
Abdu anadai majambazi hao waliokuwa wamebeba silaha mbalimbali zikiwemo mapanga na visu, yalivunja milango ya nyumba hiyo na kupora mali mbalimbali za thamani na kuwajeruhi baadhi ya ndugu zake wanaoishi hapo.
Pia yanadaiwa kumpiga na kumtesa mlinzi wa nyumba hiyo yakimtaka ayapeleke kwenye chumba anacholala Alikiba.
Hata hivyo hayakuweza kumpata Alikiba kwakuwa yaliyoeshwa kwenye chumba cha Alikiba ambaye muda huo hakuwemo. Alikiba alikuwemo ndani ya nyumba hiyo lakini kwenye chumba kingine.
Majambazi hao walifanikiwa kuiba vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na pesa taslimu shilingi milioni mbili na nusu. Picha zilizochukuliwa baada ya tukio hilo zinaonesha milango kadhaa ya nyumba hiyo ikiwa imevunjwa na uharibifu mkubwa unaonekana kufanywa.
Abdul Kiba amepost picha Instagram na kuandika: Tunamshukuru M/mungu tupo salama.
0 comments:
Post a Comment